JENGO LINAJENGWA NA MTAALAMU(CONSULTANT), MKANDARASI NI MTEKELEZAJI TU.

Katika miradi ya ujenzi wa majengo michoro huwa inafanywa na wataalamu wa usanifu majengo pamoja na wahandisi, hawa ndio wataalamu ambao kimsingi ndio wajenzi wa jengo/mradi wenyewe. Maelekezo yote na kila kinachohusika wanakuwa wamekiwakilisha kwenye michoro kwa hiyo mkandarasi au fundi anachofanya ni kutekeleza kile ambacho kimeelekezwa kwenye michoro.

MKANDARASI ASIYE WA FANI HUSIKA AKIFANYA MAAMUZI BILA KUMSHIRIKISHA MSHAURI WA KITAALAMU KAZI HUHARIBIKA

Mkandarasi au fundi anapokabidhiwa michoro anatakiwa aidha afuate kilichoelekezwa kwenye michoro na ikiwa anahitaji kufanya mabadiliko yoyote aidha kwa kufikiri mwenyewe au baada ya kushauriana na mteja, anapaswa kwanza kuwasiliana na mshauri wa kitaalamu aliyefanya michoro wakashauriana na kuelewana ndipo afanye mabadiliko hayo kwa maelekezo ya mtaalamu husika.

ANAYEJENGA NI MTAALAMU(CONSULTANT) MKANDARASI AU FUNDI ANATEKELEZA TU

Kwa mujibu wa utaratibu wa ujenzi kimsingi mkandarasi haruhusiwi kufanya tofauti na michoro bila kupata idhini ya mtaalamu aliyefanya kazi ya jengo husika kwa sababu anayejenga ni mtaalamu na sio mkandarasi kwani mkandarasi ni mtekelezaji wa kile kilichofanya na mtaalamu wa ujenzi na mara nyingi akijaribu kubadilisha kienyeji bila kushauriana na mtaalamu mambo huharibika. Japo katika miradi mingi mivutano hutokea kati ya mkandarasi na mshauri wa kitaalamu lakini mwishowe ubora wa kazi na thamanni yake huongezeka sana.

MSHAURI WA KITAALAMU ANAONGEZA SANA THAMANI YA JENGO KUKOSEKANA KWAKE KUNAPELEKEA UBORA NA VIWANGO VYA JENGO KUPUNGUA

Kazi ikiachiwa mkandarasi peke yake au fundi peke yake halafu kama mkandarasi mwenyewe au fundi mwenyewe sio mtaalamu wa fani husika ya ujenzi kwa maana ya kwamba sio msanifu majengo wala mhandisi kitaaluma basi ni rahisi kazi hiyo huweza kuwa na dosari nyingi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *