GHARAMA YA RAMANI YA UJENZI ISIWE SABABU YA WEWE KUJENGA JENGO LA HOVYO.
Wote tunafahamu kwamba ujenzi wa nyumba ni gharama sana, ni moja kati ya miradi yenye gharama kubwa sana kuifanya katika maisha ya watu wengi. Gharama ya kukamilisha nyumba moja ya kuishi ambayo sio ya ghorofa unaweza kununua hata magari 10 ya Tshs milioni 15 kila moja. Na hiyo ndio maana watu wengi wanaojenga huwa hawakamilisha mradi wote kwa mara moja, badala yake huwa wanaenda hatua kwa hatua mpaka kukamilisha.
Lakini pamoja na kwamba mradi wa ujenzi ni wa gharama kubwa sana bado watu wengi huishia kujenga majengo ya hovyo kwa kushindwa kuwaza kwa usahihi. Kwanza kabisa tofauti kati ya ujenzi bora na ujenzi wa hovyo haisababishwa na gharama ya mradi bali kushindwa kufanya maamuzi sahihi kutokana na kutawaliwa na hisia zaidi na kushindwa kuwaza kwa usahihi.
Kutawaliwa na hisia husababisha watu wengi kuwaza kwamba gharama ya ramani ya ujenzi ni kubwa sana bila kuangalia thamani ambayo inaenda kutoa na hivyo kwa hofu ya gharama kubwa watu wengi wanakwepa na kuanza kuunga unga kwenye eneo la ramani kitu ambacho hupelekea kuokoteza ramani isiyo ya viwango wala isiyokidhi mahitaji sahihi ya mteja na hivyo kuishia kuwa na jengo la hovyo ambalo hulijutia sana baadaye.
Gharama ya ramani ya jengo ni ndogo sana ukilinganisha na thamani inayotoa, yaani ramani ya jengo inayotoka miongozo yote ya kitaalamu juu ya ujenzi husika wa jengo linalogharimu zaidi ya shilingi milioni 100 haifiki hata nusu ya gharama ya kupiga jengo plasta, lakini mtu anaweza kukwepa na kuishia kuwa na jengo la hovyo kuliko hata jengo lisilopigwa plasta kabisa na baadhi ya wengine kuja kulazimika kubomoa na kurekebisha kwa majuto makubwa.
Fanya maamuzi sahihi, epuka kujenga jengo la hovyo kwa kushindwa kufikiri kwa usahihi.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!