MSIMAMIZI BORA WA UJENZI APATIKANE SAITI MUDA WOTE.

Mradi wa ujenzi ni moja ya kazi zenye vitu vingi sana kuanzia kwenye kuandaa michoro lakini zaidi katika utekelezaji wa mradi wenyewe katika hatua ya ujenzi. Hili linapelekea kwamba ili mradi utekelezwe kwa usahihi na kupunguza sana makosa unahitajika umakini wa hali ya juu sana wakati wote wa utekelezaji. Kila kitu kinachofanyika kila siku kinatakiwa kufuatiliwa kama kimefanyika kwa usahihi na kufuata mtiririko unaotakiwa na uliokubaliwa na pande zote zinazohusika na mradi huu kuanzia washauri wa kitaalamu, mteja mwenye jengo mpaka mkanadarasi husika, haijalishi ni mradi mkubwa au ni mradi mdogo kiasi gani.

KAZI KUBWA YA “SITE FOREMAN” NI KUHAKIKISHA UTEKELEZAJI WA VIWANGO VILIVYOWEKUBALIWA AU VYA JUU.

Kutoka kwenye uzoefu wa miradi mingi sana ya ujenzi tuliofanya na kusimamia tangu mwanzoni mpaka unakamilika tumeweza kugundua kwamba ili hilo liwezekane na kuondoa makosa kwa kiwango kikubwa inatakiwa awepo msimamizi mwenye uzoefu “site foreman” anayepatikana katika eneo la ujenzi kila siku na chochote kinachofanyika ni lazima akague kama kinafanyika katika viwango vilivyopitishwa na washauri wa kitaalamu wahusika wa ujenzi. Mtu huyu anapokosekana katika eneo la ujenzi muda wote na mambo mengine yakafanyika bila kukaguliwa kama yamefikia viwango vilivyopitishwa na watalaamu husika au kama yamefikia viwango vya juu vya ufundi, jengo husika lazima litakuwa na makosa mengi. Usikubali mradi wako ufanyike bila kuwepo kwa “site foreman” muda wote katika eneo la ujenzi, asikosekane hata mara moja hasa ikiwa kuna kazi inaendelea na hasa kazi mpya.

MSIMAMIZI HUYU ANATAKIWA KUPATIKANA “SITE” MUDA WOTE WA UJENZI KUEPUSHA KAZI KUHARIBIKA

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *