NENDA NA MTAALAMU KWENYE HALMASHAURI YA JIJI, MANISPAA AU MJI KUFANYA MAAMUZI SAHIHI

Unapokwenda kwenye ofisi za mamlaka za jiji, manispaa au mji ili kuweza kujua taratibu sahihi za kufuata ili kupata kibali cha ujenzi pamoja na miongozo mingine kutoka kwenye halmashauri hizo ni vyema kuambatana na mtaalamu ili kurahisisha na kuokoa muda wa kufanya maamuzi ya haraka na nini kifanyike. Watu wenye mamlaka kwenye hizi taasisi watakupa mwongozo na ushauri wa jumla wa yale unayoweza na kupaswa kufanya ili kukamilisha taratibu zinazohitajika.

KUSHAURIANA NA MTAALAMU NI MUHIMU SANA KATIKA KUFIKIA MAAMUZI SAHIHI

Lakini kutokana na uzoefu na utaalamu wake pamoja na taarifa za kutosha alizonazo mtaalamu wa ujenzi hasa kwa upande wa usanifu mtaweza kushauriana juu ya maamuzi sahihi ya kuchukua ambayo yanaendana hali halisi iliyopo na kukidhi vigezo na masharti ya mamlaka hizi. Kwenda na mtaalamu wa ujenzi katika kufahamu taratibu sahihi itakusaidia sana kwenye kuepusha kuyumbishwa na kupata uhakika wa mambo na hivyo kufanya maamuzi ya haraka na kuchukua hatua mara moja hivyo kuokoa muda, lakini pia itasaidia kuuliza maswali yote yenye utata na kupata majibu ya moja kwa moja na kufanya maamuzi sahihi mara moja.

KUEPUKA USUMBUFU NA MIVUTANO NA OFISI ZA WENYE MAMLAKA NI MUHIMU KUANZIA KWAO

Kuanzia kwenye ofisi za kwneye mamlaka zinazosimamia sheria na taratibu zote za miradi ya ujenzi ni hatua itakayokuepusha na usumbufu mkubwa unaofuata unapoanza kufuatilia kibali cha ujenzi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *