UZURI WA NYUMBA UNACHANGIWA KWA KIASI KIKUBWA SANA NA “FINISHING”.
Katika ujenzi hatua ya “finishing” tunaweza kuihesabu kwamba inaanzia katika hatua ya kupiga ripu nyumba au maarufu kama kupiga plasta. Japo uzuri wa muonekano wa jengo huchangiwa sana na ubora na umaridadi wa kazi ya usanifu iliyofanywa na mtaalamu, lakini kazi ya ujenzi kwenye utekelezaji wa kazi husika ya usanifu ina nafasi kubwa sana ya kuboresha muonekano wa jengo kutokana na ubora wa utekelezaji. Kitaalamu kuna kitu kinaitwa “workmanship”, yaani ule ubora na usahihi wa matokeo ya mwisho wa kazi ya ujenzi na “finishing” katika viwango husika.
Hatua ya “finishing” hasa kuanzia katika hatua ya kupiga ripu kuendelea ndio eneo ambalo makossa mengi yaliyofanyika nyuma yanatakiwa kurekebishwa na kulinyoosha jengo likae katika viwango sahihi kupitia kupiga ripu na nyeru. Hata pale inapotokea kazi ya usanifu haikuwa nzuri kwa mvuto au kwa umaridadi wa kazi yenyewe, lakini ikiwa kazi ya umaliziaji “finishing” itafanyika katika viwango bora na ubunifu mkubwa basi itasaidia sana kuiokoa jengo husika na kulifanya lenye mvuto sana. Hata hivyo ubora wa kazi ya umaliziaji ambao unatakiwa kufanyika kwa viwango vya juu ili kuhakikisha jengo linabaki na mwonekano bora kabisa unatokana na ubora na umakini wa wanaofanya kazi husika ukiambatana na usimamizi bora wa kazi hiyo kwa ujumla.
Hivyo inapotokea ikawa hujaridhishwa na uzuri wa mwonekano wa jengo kutokana na kukosa ubunifu wa kisanifu pamoja na umaridadi ambao uliutarajia, basi jambo la muhimu ni kuweka nguvu na umakini kwenye kazi ya umaliziaji(finishing) ambapo ikiwa itafanyika kwa viwango bora na ubunifu itaongeza mvuto wa jengo hilo kwa kiasi kikubwa.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Habari Sebastian,
Je njia gani ninaweza kutumia ili nipate makadirio ya jumla ya gharama za ukarabati wa nyumba ninayotaka kununua?.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Asante sana kwa makala nzuri