UNAFUU KATIKA UJENZI WA SHULE AU TAASISI KUBWA INAYOHUSISHA MAJENGO MENGI.
Wapo watu wengi ambao wamekuwa wakifikiria kuanzisha taasisi mbalimbali na hasa taasisi za elimu hususan shule, lakini kwa bahati mbaya changamoto yao kubwa wanayokutana nayo ni kukosa uwezo wa kufadhili miradi ya kujenga shule husika.
Kutokana na kukosa uwezo wa kujenga licha ya kuwa na kipaji cha kuendeleza shule husika watu wengi wamekuwa wakikata tamaa kwa kuona kwamba mipango yao sio rahisi kufanikiwa.
Lakini kila kitu kilichokuwa kikubwa huwa kinapaswa kufanyika taratibu hatua kwa hatua mpaka kufikia ndoto kubwa mtu aliyonayo.
Hivyo kwa upande wa huduma za kitaalamu kwenye ujenzi unaweza kutengeneza ramani ya eneo lote “master plan”, ambapo utaweka mpango sahihi unaouhitaji kwa kadiri ya mahitaji ya taasisi yake kisha utaendeleza jengo moja au machache unayoweza kumudu na kuanzisha taasisi yaek.
Kwa kuwa tayari una “master plan” utaangalia kadiri unavyozidi kufanikiwa utaanza kuendeleza majengo mengine taratibu moja baada ya jingine mpaka kukamilisha kile ulichokuwa unakiazimia mwanzoni.
“Master plan” inafanyika kwa kuzingatia vitu ambavyo vingi ni kanuni za kitaalamu ambazo zinahakikisha eneo linapangiliwa kwa usahihi kwa kuzingatia ukanda maalumu wa jengo husika.
Karibu kwa kazi zote za “master planning” kwa majengo yoyote yale hasa taasisi au maeneo makubwa ya starehe.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Nimekuelewa sana Architect Sebastian,
Kiukweli kuna shule ya sekondari ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Mmiliki wa shule hii alianza na madarasa machache kwa kufundisha masomo ya ziada (Tuition center).
Baadaye akafungua shule ya sekondari. Ni malengo na kuweka msimamo wa kusimamia malengo yako.
Asante sana kwa somo zuri.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Ahsante sana kaka.
Karibu sana sana