USIMAMIZI KATIKA UJENZI UNASAIDIA KAZI KUFANYIKA KWA HARAKA NA KWA VIWANGO.

Kwa sababu kazi ya usimamizi kitaalamu inatakiwa kufanyika kwa kufuata mtiririko maalum ulioandaliwa kupitia orodha ya mambo yanayofanyika ambayo ndio mwongozo wa mradi husika kiufundi na kitaalamu basi kazi haiwezi kusimama kwa sababu yoyote isipokuwa kama sababu yenyewe ni sehemu ya mradi husika.

Kwa sababu kazi haiwezi kusimama kutokana na utaratibu maalumu wa kiusimamizi na upatikanaji wa kila kinachohitajika kwa muda na kwa gharama sahihi kupitia usimamizi basi kazi hiyo itakwenda haraka zaidi kwa kuwa hakuna kizuizi na mradi utakamiliki kwa muda mfupi zaidi ukilinganisha na ujenzi wa kienyeji.

Usimamizi pia kwa sababu unakuwa unafuata orodha ya mambo yaliyopangwa katika utekelezaji na viwango vilivyokubaliwa bila kuruhusu kupunguza viwango vya ubora kwa sababu yoyote ile basi uhakika wa kazi ya viwango vya juu vya ubora ni mkubwa.

Karibu kwa huduma za ujenzi na usimamizi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *