USAFI WA ENEO LA UJENZI.
Katika eneo la ujenzi kunaweza kuwa na aina mbili za uchafu. Moja ni uchafu ambao unatokana na takataka zilizotokana na kitendo cha kusafisha eneo husika kutoka kwenye hali iliyokuwepo mwanzoni kama vile miti, miinuko, au aina nyingine uchafu wa eneo husika. Mbili ni uchafu ambao umeletwa na vifaa au malighafi zinazotumika kwa ujenzi husika. Aina hizi za uchafu zote zinaweza kuwa na madhara sana kwa ujenzi huo kutokana na namna athari husika zinaweza kuwa na hatari kubwa.
Ni kosa kubwa kwa eneo la ujenzi kufanyiwa usafi wa kutosha kwa sababu hilo linachangia ujenzi huo kushindwa kuwa imata vya kutosha kwani uchafu hupelekea vifaa vya ujenzi kushindwa kushikana kwa uimara wa hali ya juu kama inavyotakiwa. Hivyo kutokana na athari hizo eneo la ujenzi linapaswa kuhakikishwa kuwa linazingatia usafi na unadhifu wa hali ya juu katika kipindi chote cha ujenzi wa mradi wa jengo mpaka kukamilika.
Karibu sana.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!