NYUMBA UFUKWENI YA AUSTEN HELLER NA HOWARD ROARK.
KITABU: FOUNTAINHEAD.
AUTHOR: AYN RAND.
– Howard Roark amepata kazi kwenye kampuni ya John Erik Snyte. Anaanza kazi mara moja, siku hiyo hiyo na kukesha akifanya kazi.
– Ellsworth Toohey anaitisha mgomo mkubwa wa wafanyakazi. Ellsworth Toohey anasifika kwa msimamo na kutopokea rushwa na anakataa fedha anazotaka kupewa.
– Guy Francon anamtambulisha Peter Keating kwa binti yake anayeitwa Dominingue kisha anaondoka haraka.
– Dominingue anamwambia Peter Keating kwamba anaona wazi kwamba kinachoenda kutokea baina yao ni mapenzi. Anamwambia kwamba anaona kabisa Peter Keating anaenda kumpenda na hilo liko wazi kabisa.
– Peter Keating anamwambia Dominingue kwamba anataka kumweka kwenye wakati mgumu, Dominingue anamjibu kwamba baba yake alipaswa kumweka wazi juu ya hilo.
– Peter Keating anamsifia Dominingue kwa kufanya kazi kwenye kampuni kubwa ya habari ya Gail Wynand lakini Dominingue anamwambia haoni heshima yoyote kwa kampuni ile. Haoni kama kampuni ile inapaswa kupewa heshima hiyo kwa sababu hakuna thamani inayoisimamia.
– Dominingue anamwambia Peter Keating kwamba anampenda na kumkubali Ellsworth Toohey kwani anamsaidia kufanya kile ambacho angetamani kifanyike lakini ni kwa namna kama ya kulipa kisasi.
– Watu wanahudhuria kwenye mkutano ulioandaliwa na lakini baada ya mkutano huo Dominingue anakataa kupelekwa nyumbani na Peter Keating anamwambia kwamba kuna usafiri utamchukua.
– Guy Francon anatokea na kumwambia Peter Keating waondoke, ampeleke anakokwenda.
– Guy Francon anamwambia Peter Keating kwamba ni matumaini yake kwamba atawezana vizuri na binti yake Dominingue. Anamwambia anajua kwamba yeye ni mpiganaji hivyo hawezi kushindwa. Guy Francon anasema kwamba binti yake Dominingue ni mtata na ameshindikana na watu wengi lakini anaamini kwamba Peter Keating atamweza. Peter Keating anamjibu kwamba anatumaini kwamba atamweza.
– Howard Roark anaendelea kufanya kazi kwenye ofisi ya John Erik Snyte.
– Austen Heller ameleta kazi yake ya kusanifu nyumba yake ya ufukweni inayojengwa juu ya ukingo wa kwenye ufukwe wa bahati kwenye ofisi ya John Erik Snyte na kazi hiyo inafanywa na Howard Roark.
– Howard Roark anafanya kazi hiyo kwa umakini wa hali ya juu na anafanya kazi nzuri sana. Anatumia muda mwingi na kutuliza akili yake katika kufanya kazi hiyo ambayo anaipenda sana.
– John Erik Snyte anaamini kwamba Austen Heller ataifurahia sana kazi hiyo kwani ni kazi iliyohusisha ubunifu wa hali ya juu.
– Lakini Austen Heller anaonekana kutovutiwa moja kwa moja, haonyeshi kutekwa na uzuri na ubunifu wa jengo hilo.
– Howard Roark anakuja na kuchora chora mistari kwenye michoro ya jengo hilo. John Erik Snyte anamfukuza kazi hapo hapo mbele ya Austen Heller. Austen Heller anasema tumefukuzwa kazi wote.
– Austen Heller anamwalika Howard Roark waende kupata chakula cha mchana pamoja. Anazungumza na Howard Roark na kumwambia anataka ampe mkataba wa kisimamia ujenzi wa hiyo nyumba yake.
– Austen Heller anamshauri Howard Roark kufungua ofisi yake na kumpa hela kidogo ya kuanzia.
– Howard Roark anafungua ofisi yake mwenyewe na mradi wake wa kwanza ni mradi wa hiyo nyumba ya ufukweni ya Austen Heller.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!