KAMPUNI KUSHINDA ZABUNI YA JENGO BORA

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Kampuni ya Francon & Heyer imeshinda kwenye mradi wa Cosmo-Slotnick wa kufanya jengo lenye mvuto zaidi duniani kwa kazi iliyofanywa na Peter Keating.

2. Guy Francon anamtambulisha Peter kwamba ndiye amefanya kazi yote ya design na hivyo Peter anachukua sifa zote za umaridadi wa jengo hilo.

3. Peter Keating anapata umaarufu mkubwa sana, anahojiwa kwenye vyombo vya habari, anaandikwa kwenye magazeti na picha yake kuambatanishwa na mradi ambao ni maarufu sana pia.

4. Peter Keating anapewa mpaka nafasi ya kuwa jaji kwenye mashindano ya urembo yanayodhaminiwa na kampuni ya Cosmo-Slotnick.

5. Peter anachoma moto michoro yote iliyofanywa na Howard Roark ambayo ndio wazo la msingi la kazi hiyo kisha anaenda ofisini kwa Howard Roark na kujaribu kumpa hongo ili asije kutangaza kwamba wazo la msingi la kazi hiyo lilifanywa na Howard Roark.

6. Howard Roark anachukizwa na kitendo cha Peter kutaka kumhonga na kumrudishia pesa yake kwa kejeli. Peter anaongea maneno mengi ya kejeli kwa jazba kwa Howard Roark lakini mwishoni anaona amefanya makosa na kumwomba Howard Roark msamaha. Howard Roark anamhakikishia Peter kwamba hatazungumza chochote na kazi hiyo itabaki kuwa ni ya kwake Peter.

7. Howard Roark anapitia kipindi kigumu sana cha kifedha, anadaiwa kodi ya ofisi na bili nyingine ambazo hajaweza kuzilipa. Lakini anajipa matumaini kwamba atafanikiwa kupata mradi mkubwa sana wa Manhattan Bank Company wa ghorofa 20 ambao ameahidiwa na Mr. Weilder kwamba ataupata.

8. Howard Roark anaitwa kwenye kikao na mkurugenzi wa Manhattan Bank Company Mr. Weilder na kuambiwa kwamba mradi ameupata. Lakini anatakiwa kufanya mabadiliko kidogo ya baraza kuingiza vipengele vya usanifu majengo vya Ugiriki ya kama vile Doric columns.

9. Howard Roark anajaribu kuwashawishi kwamba hayo mabadiliko hayana tija wala msingi wowote na yataharibu ile maana halisi ya jengo hilo. Wanakubaliana naye na kumwambia yuko sahihi lakini wanajaribu kuangalia pia namna watu au umma utakavyolipokea jengo, wasipofanya kabisa hayo mabadiliko umma unaweza kulikataa.

10. Wanamshawishi Howard Roark kufanya hayo mabadiliko ili achukue huo mradi na kama hataki kuna mapendekezo mengine ya kutoa mradi huo Gordon L. Prescott. Howard Roark anapata wakati mgumu kuamua kwenye mtego huo lakini mwisho anakataa na kukubali kuukosa mradi huo.

11. Howard Roark anarudi nyumbani, kisha anaenda kufunga ofisi yake kwa sababu amekosa pesa ya kulipa kodi na kisha anakwenda kutafuta kazi za kufanya mitaani.

12. Alikutana na rafiki yake Mike ambaye alimsaidia kupata kazi hizo.

13. Sherehe kubwa inafanyika juu ya ubia mpya wa kampuni ya Francon & Heyer na wasanifu majengo mashuhuri na watu wengine mashuhuri wa fani ya Usanifu Majengo wanahudhuria. Jina la kampuni linabadilishwa kutoka Francon & Heyer kwenda kuwa Francon & Keating.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *