KUTENGENEZA MIPANGILIO YA NDANI YA JENGO (INTERIOR DESIGN).

Mipangilio ya ndani ya jengo maarufu kama “interior designing” ni kazi za kisanifu za jengo ambazo huwa mara nyingine hazionekani kama zina umuhimu mkubwa japo gharama za kutengeneza michoro yake huwa ni kubwa sana. Watu wengi huona kama wanaweza kuiga tu kokote na kuweka na kupata kile wanachotaka bila kutumia gharama kubwa sana katika michoro. Hata hivyo watu wengi zaidi wala huwa hawajihangaishi kabisa na mpangilio wa ndani (interior) bali namna vyumba vilivyopangiliwa katika mchoro wa kawaida huoni inatosha.

Lakini ukweli ni kwamba michoro ya mipangilo ya ndani ya jengo kwa mlalo na kwa wima huongeza sana thamani ya vyumba na umaridadi wake pale unapohusishwa utaalamu madhubuti. Hata kuna baadhi ya maeneo kama vile mahoteli, kumbi za starehe na hata migahawa ya kisasa ambapo utaalamu huu hauepukiki ikiwa mhusika anahitaji kuwa na mwonekano bora wenye hadhi inayoendana na ile huduma anayoitoa. Lakini hata kwa nyumba za makazi ikiwa mtu anahitaji kuifanya nyumba yake kuwa bora sana na itakayompendeza sana kuishi ndani yake akiifurahia na kuburudika basi huduma hii ya mipangilio sahihi ya ndani ni muhimu sana.

Kuna vitu vingi ambavyo vitafanyika katika viwango bora na kwa uwiano sahihi na kuongeza sana thamani ya nyumba na hususan mazingira ya ndani ya jengo ambavyo vitawezeshwa kwa viwango sahihi na utaalamu huu.

Tuwasiliane.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *