KWENYE UJENZI UFUNDI NA USIMAMIZI WA KITAALAMU NI VITU VIWILI TOFAUTI.

Baadhi ya watu wamekuwa hawaelewi sana undani wa yale yanayoendelea kwenye miradi ya ujenzi hivyo wamekuwa wakidhani kwamba wakishakuwa na fundi wa kuwajengea nyumba yao basi wanakuwa wamemaliza suala la ujenzi kwa uhakika kabisa. Lakini unapokuja kwenye uhalisia wa kazi unakuta hilo sio kweli kwani hata katika ujenzi unaozingatia taratibu rasmi zilizowekwa na mamlaka zinazosimamia ubora, viwango na taratibu mbalimbali za ujenzi zimeweka utaratibu tofauti kabisa na huo.

Kwenye taratibu rasmi za ujenzi katika miradi ya ujenzi inayofuata taratibu hizo zilizowekwa huwa kuna mkandarasi wa mradi na kuna washauri wa kitaalamu katika ujenzi. Mkandarasi katika ujenzi ndio saw ana fundi katika miradi hii midogo ya kawaida mitaani yaani yeye ndiye anayefanya kazi ya kutekeleza au kwa kiingereza wanaita(execution) ya mradi husika. Mandarasi ndiye mwenye vifaa na mashine zote na ndiye anayetazama michoro ya ramani na kutekeleza au kujenga kile kilichofanywa na wataalamu wa mradi wa ujenzi husika ambao ni kama vile mtaalamu wa usanifu wa jengo, mtaalamu wa uhandisi wa jengo, mhandisi umeme n.k., Hao ndio wanaokuwa wamefanya kazi zile za kitaalamu kisha anakuja mkandarasi ambaye ndiye kama fundi wa kujenga jengo hilo au mradi huo.

Sasa katika taratibu za ujenzi wenye maamuzi ya mwisho na wanaoamua kila kitu kifanye namna gani sio mkandarasi na timu yake bali ni wale wataalamu wa ujenzi waliofanya kazi hiyo, mkandarasi yeye anasikiliza na kufuata kile kinachoamualiwa na wataalamu waliofanya kazi hiyo. Popote utakapokuta mradi unaendelea hata ukikuta ni watu wa nje wanaufanya iwe ni wachina, wahindi au wazungu, mwenye nguvu ya maamuzi ya mwisho sio mjenzi bali ni mshauri wa kitaalamu ambapo huwa ni msanifu jengo, mhandisi jengo, mkadiriaji majenzi, mhandisi huduma n.k.,

Sasa tunapokuja kwenye miradi ya mtaani pia ili kazi ifanyike kwa viwango sahihi inapaswa kuwa na mshauri wa kitaalamu ambaye aidha ndiye aliyefanya au mwenye taaluma hiyo ambaye ndiye atakayemwongoza fundi kama jinsi mkandarasi anavyoongozwa na washauri wa kitaalamu. Fundi anapoongozwa na mshauri wa kitaalamu kwanza atafanya mambo mengi kwa usahihi kwani mshauri atakauwa anazingatia kanuni sahihi za ujenzi ambazo ni suluhisho kwa changamoto nyingi baadaye lakini hata mpangilio sahihi wa vyumba na muonekano huwa rahisi kuharibika au kuharibiwa na ufundi kama hakuna mshauri wa kitaalamu wa kufanya maamuzi sahihi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *