MRADI WA UJENZI USIOENDESHWA KWA MFUMO.

Kabla ya kujadili namna ya kuendesha mradi wa ujenzi bila mfumo au pamoja na mfumo kwanza tujadili mfumo ni nini? Mfumo maana yake ni utaratibu fulani uliopangwa ambao unafuata mchakato maalum katika ufanyaji wa mambo yake kwa kufuata mfululizo fulani uliopangiliwa. Mchakato unaofuatwa katika mfumo husika mara nyingi huwa na hatua au vitendo vinavyojirudia rudia baada ya kukamilisha mzunguko wa jambo husika au kitu husika kilichokuwa kinafanyika.

Sasa mradi wa ujenzi usioendeshwa kwa mfumo ni mradi wa ujenzi ambao haufuati mchakato fulani aua uataratibu maalum uliowekwa badala yake unafanyika kulingana na vile anavyofikiria au kuamua msimamizi wa ujenga husika. Msimamizi huyo anajiamulia mambo kulingana na uzoefu wake na ujuzi alionao na vile busara yake inamwambia bila kujali kama anaweza kuwa sahihi au la. Kwa kufanya hivyo kazi anayofanya inakuwa ni tofauti na kazi zinazofanywa na watu wengine au hata kazi mbili tofauti zilizofanywa na yeye mwenyewe zinatofautiana.

Lakini kwa kutumia mfumo, hata kazi mbili tofauti zilizosimamiwa na wasimamizi wawili tofauti kabisa, ikiwa wanafuata mfumo mmoja basi kazi hizo za ujenzi zitafanana kwa kila kitu kwa sababu wanasimamia kiwango hicho hicho. Hata hivyo faida ya kutumia mfumo katika kutekeleza mradi wa ujenzi sio tu kwamba italeta matokeo yanayofanana bali itasaidia kuhakikisha mradi unajengwa kwa viwango bora kwa sababu hatua zote zinazofuatwa zinazingatia na hivyo hakuna hatua inayoweza kurukwa na kukosekana kwake kukawa ni changamoto kwa sababu msimamizi anachozingatia ni hatua zote za kwenye mfumo zimefuatwa, ambapo zoezi hili linahakikishwa na mtu zaidi ya mmoja.

Hivyo kwa sababu kwenye miradi ya ujenzi mambo mengi husahauliwa au kurukwa kwa sababu mbalimbali na kwa makusudi mbalimbali basi ndipo hupelekea miradi hiyo kuwa katika viwango duni na hata kukosa ubora na uimara uliostahili. Kwa hiyo mradi usioendeshwa kwa kufuata mfumo fulani maalum uliozingatia mambo mengi sana mara nyingi huishia kusahaulika kwa baadhi ya vitu ambavyo huja kuoenakana mwishoni wakati tayari vilishachelewa na hivyo aidha kusababisha gharama kubwa kuvirekebisha au kushindwa kabisa kurekebisha.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *