KWENYE UJENZI UAMINIFU NDIO DAWA PEKEE KWANI UHARIBIFU UNACHELEWA KUJULIKANA.

Kwa muda sasa nimekuwepo kwenye hii tasnia ya ujenzi kwa maeneo yote kuanzia kwenye eneo la ushauri wa kitaalamu na michoro ya ramani mpaka kwenye eneo la usimamizi wa ujenzi na kujenga nimejifunza mambo mengi mbalimbali. Kiuhalisia mambo ya kujenga kwenye ujenzi ni mengi sana na huwa hayaishi, na pale unapodhani kwamba umeshajua kila kitu bali utashangazwa na mambo mengi yatayoendelea kujitokeza ambayo hukuwahi hata kuyafikiria. Hivyo ujenzi huwa hauishi kushangaza kila mtu kuanzia katika eneo la kiufundi mpaka katika eneo la tabia za watu kwenye hali mbalimbali.

Hata hivyo leo nataka nigusie eneo moja la uaminifu kwenye ujenzi. Kwanza kabisa suala zima la uaminifu katika ujenzi ni moja kati ya tabia ambazo ni mara chache sana kukosekana, watu wasio waaminifu ni wengi sana na sababu kubwa ni uwepo wa pesa nyingi na fursa nyingi za kufanya udanganyifu na ubadhirifu kwenye ujenzi. Hivyo ikiwa wewe unafanya kazi na watu bila kuwa makini nao uwezekano wa kufanyiwa udanganyifu ni mkubwa pia. Na kwa bahati mbaya zaidi wale watu unaowaamini sana au ambao wanajitahidi kujionyesha kwako kwamba ni waaminifu sana ndio mara nyingi wataishia kukuumiza na kukuliza.

Sasa kwenye hili la kuhakikisha unafanya kazi na mtu mwaminifu unapaswa ulipe kipaumbele sana kwani uaminifu hauna mbadala lakini pia katika ujenzi uaminifu ni muhimu zaidi kwa sababu mara nyingi matokeo ya kukosekana kwa uaminifu kwenye mradi wa ujenzi huwa yanakuja kuonekana baadaye sana baada ya mradi kuwa ulishakwisha na nyumba kuhamiwa na mhusika kuondoka kabisa. Lakini japo kumjua fundi sahihi aliyefanya kazi sio kazi rahisi lakini unaweza angalau kupata mtu bora zaidi ikiwa utazungumza na wale aliowafanyia kazi zao za ujenzi wakakupa ushahidi wa kiwango chake cha uaminifu mpaka uwezo wake kwenye kazi.

Kwa maana hiyo ili kuepusha majuto kutoka kwenye kazi yako mwenyewe na fedha yako hakikisha unapata mtu mwaminifu sana wa kumpa kazi au mradi wa ujenzi na kama hilo linakuwa changamoto sana kwako unaweza kuwasiliana na sisi tukasaidiana.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *