GHARAMA ZA USAJILI WA MIRADI YA UJENZI KWENYE BODI ZA UJENZI.

Wote tunajua kwamba mradi wa ujenzi unahitaji kupata kibali cha ujenzi ili kuruhusiwa na mamlaka husika kuendelea na ujenzi wa mradi husika. Lakini kwa miradi yote ya ghorofa inatakiwa kusajili kwenye bodi za ujenzi husika ili kuruhusiwa kuendelea. Miradi hii inatakiwa kusajiliwa kwenye bodi za ujenzi angalau tatu ambazo ya kwanza ni bodi ya wasanifu majengo na wakadiriaji majenzi maarufu kama AQRB(Architects & Quantity Surveyors Registration Board), pili kuna bodi ya wahandisi maarufu kama ERB(Engineers Registration Board) na tatu ni bodi ya wakandarasi maarufu kama CRB(Contractors Registration Board). Hizi ni bodi tatu kuu za ujenzi ambazo miradi ya ujenzi inapaswa kusajiliwa huko.

Changamoto kubwa sasa iliyopo ni uelewa wa watu kwa ujumla juu ya namna ya usajili wa miradi ya ujenzi katika bodi hizi na gharama zake. Kitu kikubwa na ambacho huwashtua sana watu kwenye usajili wa miradi katika bodi hizi ni gharama zake, gharama za kusajili miradi ya ujenzi katika bodi hizi huwa ni kubwa sana. Hii ni kwa sababu mtu unatakiwa kuzilipa kampuni zote zinakwenda kusimamia mradi husika sambamba na kununua stika kutoka kwenye bodi hizo ambazo ndio inakuwa kama malipo ya gharama za mradi husika kwa bodi hiyo ambayo ina kazi ya kusimamia taaluma husika kufanyika katika viwango sahihi. Hivyo kuyalipa makampuni manne pamoja na kulipa gharama za kwenye kila bodi husika wastani wa gharama huwezi kuwa kuanzia milioni 7 kwa madirio ya chini mpaka milioni 10 kwa mradi mdogo zaidi au wa wastani. Hili limekuwa ni jambo la kushangaza sana kwa wateja.

Lakini tofauti na kibali cha ujenzi ambacho mtu unaomba na kupata kutoka kwenye halmashauri ya jiji, manispaa au mji ambacho unalipia gharama moja tun a mara moja baada ya kupeleka michoro ya ujenzi wa jengo husika, gharama za kusajili mradi kwenye bodi za ujenzi zinahusisha makampuni mengi na stika nyingi. Lakini ikiwa mtu unatafuta namna ya kupunguza gharama hii unaweza kutafuta mtaalamu mkajadiliana akaona kile mtakachoweza kufanya angalau kupunguza mzigo huo mzito sana. Wataalamu wanaweza kukushauri njia mbalimbali za halali za kutumia uwezo kupunguza gharama hizo ambazo huisha baada ya ujezi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *