UMUHIMU WA USIMAMIZI WA KITAALAMU KWENYE UJENZI

Kutokana na changamoto nyingi, utata kwenye swala zima la ujenzi, usimamizi wa kitalaamu katika ujenzi unachukua nafasi muhimu sana katika kuhakikisha ubora na umakini wa ujenzi husika. Usimamizi wa kitaalamu umekuwa ndio injini ya huduma za ujenzi.

Usimamizi wa kitaalamu umekuwa ndio injini ya huduma za ujenzi

Baadhi ya wateja wa huduma za ujenzi wamekuwa wakitumia zaidi  njia ya kuweka fundi bila usimamizi wowote wa kitaalamu hata kama ni wa mara chache kwa wazo kwamba wanapunguza gharama bila kujua kwamba huduma ya usimamizi wanayopata ina thamani kubwa sana kuliko hiyo gharama wanayoogopa na mara nyingi itawaepusha na hasara ambayo inaweza kujitokeza kwa kukosa usimamizi.

Thamani inayoletwa na usimamizi wa kitaalamu ni kubwa kuliko gharama utakayotaka kukwepa, yaani wewe ndiye utakayenufaika zaidi.

Hizi ni baadhi ya faida zinazoletwa na kuwepo kwa usimamizi makini wa kitaalamu.

  • Usimamizi wa kitaalamu unahakikisha ubora wa jengo kwani  kuna viwango ambavyo msimamizi anasimamia ambavyo kwa uwepo wake haviwezi kushuka chini ya hapo lakini kukosekana kwake lolote linaweza kutokea.
  • Usimamizi wa kitaalamu unaokoa muda wa ufuatiliaji wa kila kitu hasa kwa upande wa mteja ambavyo inamchukua muda mwingi sana na bado hataweza kutokana na kukosa utaalamu na uzoefu bado kuna vitu vinaweza kuharibika licha yay eye kufuatailia kwa ukaribu.
  • Usimamizi wa kitaalamu unaepusha usumbufu mwingi ambao mteja anapaswa kuuingia kwa kufuatilia kila kitu na kwa sababu ya kukosa utaalamu na uelewa mpana wa mambo husika anaweza kusumbuka sana kwa vitu ambavyo havina ulazima wa kusumbuka au vinavyoeleweka kiurahisi kitaalamu.
  • Usimamizi wa kitaalamu uko kwenye nafasi nzuri na sahihi zaidi ya kukabiliana na mamlaka husika na hata kujadiliana nao, kutoa majibu ya maswali yanayoulizwa au kutekeleza maagizo yao kwa urahisi kutokana na uelewa na uzoefu walionao kuliko mteja ambaye anaweza kuyumbishwa sana na kupewa adhabu kubwa kwa vitu ambavyo vingeweza kutatuliwa kwa namna nyingine rahisi.
  • Usimamizi wa kitaalamu ndio unaobeba dhamani ya mradi husika kwa kuingia mkataba na mteja hivyo umakini unakuwa juu sana huku usimamizi ukifanya kazi kubwa ya kuzileta pamoja rasilimali zote na kuhakikisha matokeo sahihi yanayotazamiwa yanafikiwa.
USIMAMIZI UNABEBA DHAMANA YA MRADI

N:B Gharama za usimamizi au usimamizi kwa ujumla ziko chini ukilinganisha na faida unayokwenda kuipata kwa kuweka msimamizi sahihi na muhimu zaidi ni kukwepa kuja kujilaumu kwa makossa mengi na hasara utakayoingia kwa kukosekana usimamizi wa kitaalamu.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *