UJENZI BORA UNAJUMUISHA VITU VINGI

Watu wengi wamekuwa hawapati matokeo wanayoyatarajia linapokuja suala la ujenzi kwa sababu wanapofikiria kuhusu ujenzi hawafikirii kwa mapana yake badala yake wanafikiria mambo machache kwa juu juu.

Lakini linapokuja suala la ujenzi ili uweze kupata matoke bora na ya viwango vya juu kuna mambo mengi yanatakiwa kuhusika kama ifuatavyo;

WATU WENGI HAWAFIKIRI KUHUSU UJENZI KWA USAHIHI

-Jambo la kwanza ni utaalamu sahihi, kabla hujaanza kujenga lazima ufikirie namna utapata utaalamu sahihi wa kukushauri namna ya kufanikisha kwa usahihi zaidi matokeo unayoyatarajia na yapatikane kwa ubora zaidi ya vile unavyofikiria wewe. Mtaalamu huyo anaweza kuwa msanifu majengo pekee au pamoja na mhandisi na mkadiriaji majenzi.

Hili linajumuisha kutafuta mtaalamu bora wa ujenzi ambaye utamjulisha lengo na mategemeo yako sambamba na kumpeleka kwenye eneo unalotaka kujenga kisha mkajadili kwa kina kila kitu kuhusu mradi husika yeye akakushirikisha utaalamu na uzoefu wake pamoja mambo yote yanayohusisha taaluma ya ujenzi na sheria za mamlaka husika.

UJENZI BORA UNAHUSISHA KUPATA MATOKEO BORA ZAIDI YA MATARAJIO YAKO

-Baada ya hapo itahitajika kutengenezwa ramani sahihi ambayo itazingatia malengo yako, matamanio na taratibu nyingine za kitaalamu kulingana na matakwa ya mradi husika.

-Baada ya ramani kinachofuata ni usimamizi sahihi wa mradi husika, hii ni baada ya kuwa umechukua vibali vya ujenzi vinavyohitajika kutoka kwenye mamlaka husika. Usimamizi wa mradi ni sehemu muhimu sana ya kuhakikisha ujenzi unakuwa bora kwani usimamizi sahihi ndio unaozileta pamoja rasilimali sahihi kuanzia malighafi mpaka nguvu kazi kuhakikisha matokeo yanayotarajiwa yanafikiwa kwa viwango vya juu kabisa. Kukosa usimamizi sahihi kutapelekea changamoto nyingi za kitaalamu na makosa mengi ambayo yanaweza kuleta hasara kubwa au matokeo mabovu.

USIMAMIZI SAHIHI NDIO KITU MUHIMU ZAIDI KATIKA UJENZI BORA

-Ujenzi bora unahitaji uzoefu, uzoefu na utaalamu ndio chachu ya ubora na utatuzi wa changamoto nyingi sugu na zisizotarajiwa. Kuna changamoto nyingi zisizotarajiwa ambazo ni vigumu hata kufikiriwa mwanzoni mwa mradi ambazo hutokea mara kwa mara ambazo hata utaalamu peke yake hautoshi kukabiliana nazo na badala ya uzoefu ndio huweza kukabiliana nazo kuhakikisha kwamba kila kitu kinaendelea kama kilivyopangwa, hivyo ni muhimu kuchagua mtaalamu mzoefu katika hili.

-Ujenzi bora unahitaji uelewa mpana kwa pande zote mbili, yaani kuwepo mashauriano na maelewano kisha makubaliano ya pamoja kwa pande zote mbili. Kukosekana kwa maelewano na makubaliano kati ya mteja na mjenzi kunachangia sana ujenzi kuwa wa hovyo na mradi kutofikia matarajio yaliyowekwa.

MAELEWANO KATI YA MTEJA NA MJENZI NI MUHIMU SANA KATIKA KUFANIKISHA MATOKEO YANAYOTARAJIWA

-Ujenzi bora unahusisha pia matumizi sahihi ya eneo husika la ujenzi ambayo yatazingatia kuanzia jiografia yake, vitu(features) vilivyolizunguka eneo yaani maeneo ya jirani pamoja na uelekeo sahihi wa jengo.

-Ujenzi bora unahusisha pia uchaguzi wa malighafi sahihi za ujenzi kulingana na malengo ya mradi lakini mara zote zinatakiwa kuwa zenye ubora sana na zinazoendana kwa usahihi na kile zinazolenga kukifanikisha

UJENZI BORA UNAHUSISHA UCHAGUZI SAHIHI WA MALIGHAFI ZINAZOHITAJIKA

NB. Ili kufanikisha ujenzi bora ambao hautakupa majuto baadaye ni lazima kuna vigezo hivi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *