GHARAMA ITAKUWA KUBWA ZAIDI YA ILIVYOPANGWA.

Kwa kawaida katika miradi ya ujenzi huwa ni vigumu sana bajeti iliyopangwa kumaliza kazi bila nyongeza ya zaidi licha ya kujitahidi kupiga mahesabu kwa usahihi mkubwa.

NI VIGUMU KUFANYIA MAKADIRIO YA GHARAMA KWA USAHIHI WA 100%, MARA NYINGI MABADILIKO HUTOKEA

-Hili hutokea kwenye miradi ya aina zote kwa sababu ni mara chache sana kuweza kutabiri kila kitu kwa usahihi kuanzia muda utakaotumika, dharura zitakazotokea na mabadiliko ya bei za vifaa na gharama nyingine vinavyotokea kila siku.

-Hivyo unapopanga bajeti katika mradi wako wa ujenzi hupaswi kuamini kwa asilimia mia kwamba hiyo ndio gharama itakayotosha kila kitu bali weka kichwani kama kwamba huenda kukawa na ongezeko kidogo la gharama na ujiandae kabisa kwa dharura.

-Lakini pia mara nyingi, karibu mara zote wakati ujenzi unaendelea mabadiliko hujitokeza au mapendekezo mapya madogo madogo aidha yaliyoamulia na wewe binafsi au yaliyotokana na sababu za kiufundi ambayo huongeza gharama pia.

MABADILIKO YA GHARAMA HUTOKEA KARIBU MARA ZOTE NA KWA MIRADI YA AINA ZOTE

NB: Ongezeko la gharama zaidi ya iliyopangwa kwenye ujenzi ni jambo linalotokea karibu mara zote, na hili sio kwa miradi ya watu binafasi peke yake bali mpaka kwenye miradi ya taasisi binafsi na kwenye miradi ya mashirika na taasisi za kiserikali.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *