KULAZIMISHA BEI NDOGO NI KULAZIMISHA HUDUMA MBOVU.

Wengi wetu, kutokana na mazoea na hisia zilizotutawala kila tunapofikiria kuhusu huduma za kulipia huwa tunakimbilia kufikiria ni wapi tutapata kwa bei ndogo. Lakini kwa uzoefu mkubwa tuliopitia tumeweza kuona uhalisia wake katika utekelezaji wa ile huduma husika hupelekea matokeo yasiyotarajiwa karibu mara zote.

KULAZIMISHA BEI YA HUDUMA ISIYO SAHIHI HUPELEKEA MATOKEO YASIYOTARAJIWA KARIBU MARA ZOTE

-Kwanza kabisa wale watu wenye uwezo mkubwa na maarifa sahihi ya huduma husika watakukatalia kufanya kwa bei ambayo iko chini ya viwango vya kawaida hivyo mbadala utakaobaki nao ni watu wenye uwezo wa kawaida na uwezo wa chini.

-Pili hutakosa wa kukufanyia kwa bei unayotaka. Ingekuwa na afadhali kama utakosa mtu wa kukufanyia kwa bei ya chini sana na kuharibu kazi kisha ukalazimika kumfuata wa bei sahihi na kupata huduma sahihi ambayo hutaijutia. Lakini kwa bahati mbaya ni kwamba hutakosa wa kukufanyia kazi kwa bei ya chini sana kwa kadiri uwezo wake utakapoishia lakini atakufanyia kazi ambayo mwishoni utaIjutia.

HUTAKOSA MTU WA KUKUFANYIA KWA BEI YA CHINI SANA LAKINI ATAKUFANYIA KWA KADIRI YA UWEZO WAKE UNAPOISHIA NA MARA NYINGI UTAKUJA KUYAJUTIA MATOKEO

-Iwe ni huduma ya michoro au huduma ya kusimamia ujenzi lakini sababu ya watu wenye uwezo kukukatalia ni kwa kuwa bei unayojaribu kulazimisha hailingani na thamani ya mradi unaoenda kujengwa na kukosekana kwa uwiano namna hii kutapelekea kazi husika kufanyika kwa chini ya viwango hivyo mtu mwenye uwezo anakuwa anakwepa kuharibu sifa yake kwa kukubali kufanya kitu kitakachokuwa na matokeo ya chini ya viwango vyake au matokeo mabovu.

– Unapotaka kujenga mara zote jaribu kutafuta uwiano kati ya gharama zote za kujenga jengo zima mpaka kukamilika na gharama unazokwenda kuwalipa wale wanaokupa huduma zote za ujenzi kwa sababu ili kufanikisha kupata matokeo ambayo hutayajutia unatakiwa kuona uwiano katika hili.

TAFUTA UWIANO KATI YA GHARAMA ZA MRADI MZIMA NA BEI ZA HUDUMA WANAZOTOA WATAALAMU

Mwisho wa siku endapo utalazimisha bei ya chini sana hata kama uliyempa kazi hiyo ni mtu mwenye uwezo na uzoefu, bado kuna nafasi kubwa ya kuja kumlaumu baadaye kwa sababu yeye atakuwa ameongozwa zaidi na tamaa japo akili yake haikubaliana na bei husika na matokeo yake ni kushindwa kutoa huduma yenye ubora ulio katika viwango sahihi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *