MICHORO YA RAMANI KUCHELEWA KUKAMILIKA.

Wateja wengi wamekuwa wakishangazwa na kwa nini kazi ya michoro inachukua muda mrefu sana kukamilika tofauti na matarajio yao na saa nyingine hasa kuvuka ile tarehe ya makubaliano kwamba michoro itakuwa tayari.

Kuna sababu mbalimbali ambazo hupelekea michoro kuchelewa, nyingine zikiwa sababu za msingi kidogo lakini nyingi zikiwa sio sababu za msingi kwa michoro kuchelewa. Hata hivyo sababu kubwa kabis aya kazi kuchelewa mara nyingi huhusiana na fedha na hasa namna ya ulipaji.

Kwa mfano kwa mradi ambao pesa haijalipwa kabisa hata ile “advance payment” mtaalamu hutafsiri kwamba huo sio mradi na hivyo hautakiwi kupewa kipaumbele na kuupuzia hivyo kuuchelewesha, lakini pia kwa mradi ambao fedha yote imelipwa kwa mara moja inaweza kumfanya yule mtaalamu kama sio mtu mwaminifu akatumia pesa yote kisha hamasa ya kufanya ile kazi ikaondoka na hivyo kujivuta sana kukamilisha kazi husika.

Hivyo ni muhimu kujua hizi motisha zinazopelekea kazi kuwahi au kuchelewa na hata ubora wa kazi zenyewe kupitia hizi mbinu za ulipaji wa fedha za mradi husika.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *