KAMA UNAHITAJI KAZI UTAKAYOIPENDA HAKIKISHA UNASHIRIKI KWENYE KILA HATUA.

Ikija suala la nyumba ya mtu au mradi wake wa ujenzi watu huwa wamegawanyika katika kkiwango cha kujihusisha na mradi husika. Kuna wateja ambao huwa wanashiriki kikamilifu sana, kufuatilia kila kitu na kuuliza maswali mengi zaidi na kutoa maoni na msimamo wao. Lakini kwa upande mwingine kuna wateja ambao sio wapenzi wa kuingilia sana kazi yake ya ujenzi badala yake anamsikiliza mtaalamu kila kitu na kumtegemea kwamba atafanya kwa usahihi zaidi bila kuingiliwa.

MTEJA ANAPASWA KUSHIRIKI KWENYE KILA HATUA YA MRADI WAKE NA KUZUNGUMZA MAONI NA MATAMANI YAKE

Ni kweli kwamba mtaalamu anapopata uhuru wa kutosha anakuwa kwenye nafasi ya kufanya vizuri zaidi kuliko kupangiwa sana lakini inatakiwa mtaalamu anapomaliza hatua fulani ya kazi mteja aifanyie tathmini na kutoa maoni yake na matamanio yake na hapo mtaalamu ajaribu tena kuyafanyia kazi au kutoa ushauri sahihi kwa mteja katika kufanikisha mambo hayo kwenye mradi husika. Mteja ana haki ya kupata ufafanuzi wa kutosha kwenye kila kitu kinachomtatizo au kumshangaza na hapo naye aweke mchango wake katika kufanikisha kile anachotamani.

Kwa ushirikiano huu na baina ya mteja na mtaalamu huku mteja akijitahidi kuhakikisha anaeleza kwa usahihi kile anachotaka na kueleweka huku mtaalamu akijitahidi kuhakikisha mteja anafanikisha lengo lake na kuridhika basi matokeo ya mwisho yatakuwa yenye ubora sana kwa mteja.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *