UMUHIMU WA KUTEMBELEA ENEO LA UJENZI KABLA YA KUANZA KUTENGENEZA RAMANI

Sio mara zote huwa ni lazima ufike eneo la ujenzi ndio uweze kutengeneza ramani ya jengo hasa kama eneo lenyewe ni mbali sana na haliwezi kufikika kiurahisi lakini ni muhimu kuhakikisha kwamba taarifa unazopewa ni sahihi ili uweze kufanya kazi ya kutengeneza ramani kwa usahihi.

KULIFAHAMU ENEO LA UJENZI KWA USAHIHI NI MUHIMU KABLA YA KUANZA KUTENGENEZA RAMANI YA JENGO HUSIKA

Lakini kama eneo lenyewe la ujenzi lina utata kidogo na hasa kama linaweza kufikika vizuri ni muhimu sana kufika kwanza eneo husika kabla ya kuanza kutengeneza ramani ya jengo lenyewe. Kufika eneo la ujenzi kutasaidia kwanza kuona site katika uhalisia na kulinganisha na vipimo vyake husika au kuchukua vipimo ikiwa bado halijapimwa. Kufika eneo la ujenzi pia kutasaidia kuelekewa uelekeo sahihi zaidi ambao unaweza kuruhusu jengo husika kuelekea(building orientation) kutokana na namna mazingira yenyewe yalivyokaa au uwepo na ufanano wa majengo mengine katika eneo la ujenzi. Kufika eneo la ujenzi pia kutakupa fursa ya kujua hali na aina ya udongo  na kama kuna chochote kinachoweza kusaidia katika kuongeza au kupunguza uimara wa jengo husika au changamoto yoyote inayoweza kuwa kikwazo kwa jengo husika.

MTAALAMU ATAKAPOSHINDWA KUFIKA ENEO LA TUKIO ATATAKIWA KUPATA TAARIFA ZOTE MUHIMU ZA ENEO HUSIKA KWA USAHIHI.

Hivyo ikiwa eneo la ujenzi linaweza kufikika kiurahisi ni muhimu mtu kufika na kuweza kuona uhalisia wa mambo yote muhimu mtaalamu anayohitaji kuyafahamu katika eneo la ujenzi, lakini ikiwa kwa sababu zozote zile mtaalamu atashindwa kufika eneo la ujenzi basi anatakiwa kupata taarifa zote muhimu za eneo la ujenzi kwa usahihi. Tutajadili taarifa hizo kwenye makala inayofuata.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *