KUJENGA KIWANJA CHA KWENYE MWINUKO NI FAIDA ZAIDI

Baadhi ya watu na hasa watu miaka ya nyuma wamekuwa wakiogopa sana viwanja vya kwenye mwinuko ambapo wengi wamekuwa wakihofia kwamba gharama za ujenzi wa kiwanja cha kwenye mwinuko ni kubwa na pia pengine sehemu iliyoinuka sio nzuri sana kwa kujenga. Hata hivyo bado mpaka sasa kuna watu wengi wenye mtazamo hasi sana juu ya ujenzi kwenye kiwanja kilichopo kwenye mwinuko kwa sababu mbalimbali ikiwemo mtazamo hasi juu ya kiwanja cha kwenye mwinuko.

KUMEKUWA NA MTAZAMO HASI SANA NA UPOTOSHAJI JUU YA KUJENGA NYUMBA KWENYE ENEO LA MWINUKO

Kuna faida nyingi sana kujenga kwenye kiwanja cha kwenye mwinuko ili mradi tu iwe ni sehemu inayofikika kwa barabara ya gari na kuna upatikanaji wa maji. Kwenye suala la gharama za ujenzi ni kweli kwamba kutakuwa na ongezeko dogo la gharama hasa kwenye hatua ya msingi wa jengo lakini hiyo ni gharama ndogo sana ukilinganisha na gharama ya jengo ambapo sio gharama inayostahili hata kuifikiria ikiwa utafikiria faida nyingine za kujenga kwenye mwinuko. Muhimu sana kujenga kwenye mwinuko ni unakuwa kwenye nafasi ya kutazama maeneo mengi kwa urahisi(mwonekano/view) huku ukipata hewa ya kutosha na mwanga zaidi kwa sababu hakuna kinachokuzuia. Kujenga kwenye mwinuko pia kunakupa fursa ya kufurahia mwonekano bora wa jengo lako hata ukiwa mbali ikiwa ulijitahidi kutengeneza jengo lenye kuvutia vya kutosha. Kujenga kwenye mwinuko kutakusaidia kupata upepo wa kutosha na hali ya hewa nzuri ndani ya jengo ukiwa kwenye miji ya joto hasa miji ya Pwani na hivyo kuepuka karaha za kuishi kwenye miji ya joto au miji yenye msongamano na kama mwinuko ni mkubwa unaweza kupata sakafu ya chini ya ardhi(basement floor) ya jengo ambayo unaweza kuitumia kwa namna nyingi.

IKIFANYIKA KAZI NZURI HASA KWENYE KUANDAA MICHORO YA RAMANI JENGO LA KWENYE MWINUKO HUWA LA KIPEKEE SANA.

Unahitaji kupata mtaalamu atakayekufanyia kazi bora na yenye kuvutia sana ikiwa unajenga kwenye mwinuko ili uweze kutumia vizuri fursa hiyo ya kujenga kwenye eneo lenye mwinuko.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *