VITU VITATU MUHIMU KATIKA JENGO LOLOTE.

Kazi nyingi za usanifu majengo zimekuwa zikifanywa na wasanifu mbalimbali huku kukiwa na kanuni za aina mbalimbali za namna gani jengo liwe au lisiwe. Hata mamlaka za kiserikali zinazoshughulika na taaluma ya usanifu majengo kuna vigezo huweka ambavyo ndivyo vinapaswa kutimizwa ili jengo likubalike kwamba linaweza kuendelea kujengwa japo vigezo hivi vinaweza kuwa katika makundi tofauti tofauti. Lakini katika hali ya kawaida kuna vitu vitatu muhimu sana ambavyo jengo lolote likiwa limevitimiza linakuwa katika usahihi mkubwa sana.

UIMARA WA JENGO NI MUHIMU SANA KATIKA KUHAKIKISHA JENGO LINADUMU NA KUEPUSHA MAAFA

Kwa mujibu wa msanifu majengo na mhandisi wa Rumi ya kale kati ya mwaka 80 KK na mwaka 15 KK, aliyejulikana kama Marcus Vitruvius Pollio au kwa kifupi Vitruvius ambaye alikuwa msanifu mashuhuru wa majengo mengi ya Rumi ya kale na aliyetoa miongozo na kanuni zilizotumika kwa majengo mengi ya miaka ya baadaye katika Rumi ya kale na hata katika nyakati nyingine zilizofuata katika vitabu vingi alivyoandika amesisitiza kanuni moja maarufu ya vitu vitatu muhimu zaidi katika jengo lolote. Kwa mujibu wa Vitruvius vitu vitatu muhimu katika jengo lolote ni “uimara”, “matumizi” na “uzuri”. Jengo lolote linapokuwa na haya mambo matatu muhimu sana linakuwa kwenye nafasi ya kuwa katika usahihi mkubwa.

MPANGILIO SAHIHI WA KIMATUMIZI UNATIMIZA MALENGO MUHIMU LA WATUMIAJI WA JENGO

Uimara ni muhimu katika kuhakikisha jengo linadumu na kuepusha maafa na hasara, matumizi ni muhimu kuhakikisha jengo linawafaa watumiaji na linatimiza lengo husika na uzuri ni muhimu kwa sababu binadamu tumeumbwa kufurahia na kujisikia vizuri kutumia vitu vizuri na vyenye kuvutia, kitu kisichokuwa na mvuto kinaua sana hamasa ya watu wanaokitumia, hivyo uzuri unaongeza hamasa zaidi ya watumiaji wa jengo husika na hata watu zaidi kuvutiwa kutumia jengo husika.

UZURI NA MVUTO WA JENGO UNAONGEZA SANA HAMASA KWA WATUMIAJI

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *