HATUA TATU MUHIMU KATIKA MCHAKATO WA KUSANIFU RAMANI YA JENGO.

Hatua ya kwanza na pengine muhimu zaidi katika mchakato mzima wa kusanifu ramani ya jengo ni kutengeneza wazi(conceptual design). Hii ni hatua ya mwanzoni kabisa ambapo mtaalamu wa usanifu anatengeneza wazo la namna ramani ya sakafu ya jengo itakavyokaa kuanzia ya chini kabisa kama jengo ni ghorofa ambapo inaonyesha mpangilio wa mtumizi ndani ya jengo, uelekeo wa jengo, uhusiano wa jengo na eneo la ujenzi pamoja na vitu vilivyolizunguka jengo, ukubwa wa jengo lenyewe, eneo na bustani zinazozunguka jengo lenyewe n.k. Baada ya hatua hii kutahitajika mjadala kati ya pande zote zinazohusika na mradi huu wa jengo kutoa maoni na mapendekezo kisha msanifu kuendelea na kazi huku akifanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa kabla ya kwenda hatua inayofuata.

BAADA YA HATUA YA KWANZA PANDE ZOTE HUKUTANA KWA AJILI YA KUTOA MAONI NA MAPENDEKEZO

Hatua ya pili muhimu katika mchakato wa kusanifu ramani ya jengo ni kutengeneza mwonekano wa jengo katika picha za pande tatu(3D views). Katika hatua hii mtaalamu wa usanifu anaendelea na usanifu wa jengo kwenye suala la muonekano ambapo japo kwa sehemu kubwa muonekano unaamuliwa na namna ile ramani ya sakafu(floor plans) ilivyokaa lakini msanifu anaweza kuongezea vitu vingine ambavyo vitapelekea mabadiliko kidogo kwenye ramani ya sakafu(floor plans). Hatua hii ni muhimu na kubwa kwani ndio itakayotazamwa zaidi na kuhukumiwa sana hata na watu wasiolitumia jengo.

JENGO LITAHUKUMIWA ZAIDI NA WATU KUTOKANA NA MUONEKANO WAKE

Hatua ya tatu muhimu katika mchakato mzima wa kufanya usanifu wa ramani ya jengo ni hatua ya kuandaa michoro ya ramani zitakazotumika katika ujenzi zikiwa kwenye vipimo vilivyoonyeshwa kwa usahihi na kujumuisha kila taarifa muhimu inayohitajika(detail drawings). Hatua hii ni muhimu sana kwani ndio inayotoa mwongozo kwa wakandarasi na wajenzi juu ya utekelezaji wa mradi katika vipimo sahihi.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *