USANIFU MAJENGO KATIKA NYAKATI ZA MESOPOTAMIA TANGU MIAKA 5,100 ILIYOPITA

Mesopotamia ni eneo la Asia magharibi lilikuwepo katikati ya mito ya Tigrisi na Yufretsi likiwa kati ya maeneo ya mwanzo kabisa duniani kuwa chanzo cha ustaarabu katika mambo nyanja nyingi za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kisayansi mpaka unajimu. Eneo la Mesopotamia kwa dunia ya leo limejumuisha nchi yote ya Iraq ya leo pamoja na sehemu za maeneo ya nchi za Iran, Uturuki, Syria na Kuwait. Eneo hili lilianza kuendeleza mawazo mbalimbali ya usanifu majengo tangu miaka 12,000 iliyopita nyakati za niolitiki wakati wa mapinduzi ya kilimo na mapinduzi makubwa ya usanifu majengo pamoja na ustaarabu mwingine yaliendelea kukua kwa kasi sana tangu miaka 5,100 iliyopita. Kwenye suala la makazi eneo hili la Mesopotamia lilikuwa ni eneo la mwanzoni sana duniani kuendeleza suala la mipango miji katika himaya hii na mawazo mengi kuhusu suala la mipango miji kuibuka. Kutokana na maendeleo ya imani za kidini pia Mesopotamia iliendeleza fani ya usanifu majengo kwa kujenga mahekalu makubwa sana sambamba na sanamu mbalimbali za wafalme na alama nyingine zenye umuhimu mkubwa katika imani za dini.

MIPANGO MIJI KATIKA MIJI YA MESOPOTAMIA YA KALE

Utamaduni wa kujenga mahekalu makubwa kwa ajili ya ibada za kidini katika himaya ya Mesopotamia ulipelekea kukua kwa utamaduni wa kujenga majengo makubwa yaliyojulikana kama zigurati yaliyokuwa makubwa sana na kujengwa kwa muundo wa kupungua kidogo ukubwa kadiri yanavyokwenda juu na pale juu kabisa ya zigurati lilijengwa hekalu kubwa ambalo watu waliamini kwamba ndio makazi ya Mungu anapoishi na watu pekee walioruhusiwa kufika hapo ni makuhani na watu wenye heshima kubwa sana katika jamii. Watu walisherehekea sana mahekalu haya na kutengeneza sanamu muhimu zilizoenda kuwekwa kwenye mahekalu haya. Hata hadithi ya mnara wa Babeli unaozungumziwa kwenye biblia takatifu wanahistoria wengi wanauhusisha na zigurati lililojulikana kama zigurati la etemenanki katika Babeli ya kale ambalo wakati himaya ya Babeli ilipokuwa mashuhuri na yenye nguvu sana mfalme Nebukadnezza wa Babeli ya kale alipanga kulijenga upya na kuliimarisha kama mnara mpya wa Babeli.

ZIGURATI LA “CHOGHA ZANBIL” LILILOJENGWA KATIKA NYAKATI ZA MESOPOTAMIA MIAKA 3150 ILIYPITA LILILOPO KATIKA NCHI YA IRAN YA LEO

Usanifu wa majengo wa staili ya zigurati iliendelezwa sana katika Mesopotamia ya kale ya kwenye himaya nyingi zaidi zilizofuatia baada ya Mesopotamia ya kale. Maendeleo ya imani pia yaliongeza ushawishi kwa himaya nyingi kujenga mahekalu makubwa kama mapiramidi ya Misri pamoja na majengo mengine muhimu kwenye jamii kama vile majumba makubwa ya kifalme na makaburi makubwa ya wafalme kwa staili kama ya zigurati kwenye himaya nyingine za kale na kuendelea mpaka sasa. Sehemu kubwa ya ujenzi katika Mesopotamia ya kale ulifanyika kwa kutumia matofali ya kuchoma ambapo kuna majengo mengine yapo mpaka leo na yamejengwa tangu takriban mpaka miaka 5,000 iliyopita.

MCHORO WA ZIGURATI NA NAMNA LINAVYOFANYA KAZI

Usanifu wa majengo wa nyakati za Mesopotamia umekuwa chanzo cha mawazo mengi mapya kisanifu katika majengo mbalimbali ya usanifu majengo na hata mipango miji maeneo mbalimbali licha ya kwamba yamekuwa na changamoto zake pia, lakini pia usanifu majengo wa aina Mesopotamia umechangia kuongeza urembo na vipengele zaidi vya umaridadi wa majengo katika ujenzi wa kisasa na kuvutia kama vile staili ya geti la Ishtari lenye umaarufu mkubwa lililojengwa miaka 2596 iliyopita kwa amri ya Mfalme Nebukadneza wa Babeli ya kale.

JENGO LA OFISI YA WAZIRI MKUU LA NCHINI IRAQ YA LEO LILILOJENGWA KWA MUUNDO WA ZIGURATI MWAKA 1975

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *