UKUBWA WA KIWANJA UNAOTOSHA KUMUDU NYUMBA YA VYUMBA VITATU.

Nimekuwa nikipigiwa simu mara kwa mara na watu wakijaribu kuuliza na kujua kama kiwanja chake kinaweza kutosha nyumba ya ukubwa fulani pamoja na matumizi mengine anayotaka kufanya katika kiwanja hicho.

Ni kweli kwamba sio rahisi kujua haswa kiwanja husika kinaweza kumudu matumizi mengi kiasi gani kwa sababu ukubwa wa matumizi ya ndani ya kiwanja ni suala la uwiano zaidi na sula la uwiano ni wa kufikirika sana haswa kuendana na mazoea na uzoefu wa mhusika.

NYUMBA YA VYUMBA VITATU

Naweza kusema kwamba nyumba ya vyumba vitatu inahitaji angalau eneo la mita za mraba 400 yaani wastani wa ukubwa wa mita 20 upana na mita 20 urefu kwa ajili ya kuweka nyumba ya vyumba vitatu ya ukubwa wastani pamoja na kupata eneo la maegesho ya magari angalau mawili mpaka matatu, eneo dogo la bustani ambalo mtu anaweza hata kufanyia shughuli ya kijamii, nyumba ndogo ya mfanyakazi, sehemu ya kuanika nguo na nyumba ndogo ya mbwa au mabanda ya kuku.

Ukweli ni kwamba eneo la kiwanja lenye ukubwa wa pungufu ya mita za mraba 300 linaweza kutosha kumudu nyumba ya vyumba vitatu lakini changamoto ni kwamba itakuwa vigumu kufanya matumizi mengine ya ziada katika kiwanja hicho. Kwa mfano unaweza kuwa na eneo la maegesho ya gari moja peke yake litakoloweza kuegeshwa bila usumbufu, pamoja na banda la mbwa peke yake.

MPANGILIO WA NYUMBA NA MATUMIZI MENGINE KWENYE KIWANJA

Lakini ikiwa kama unahitaji kujibana uwezavyo au labda ni nyumba ya mpangaji pekee na unaona huna haja ya kuacha eneo la ziada kwa ajili ya chochote basi hata eneo la ukubwa wa mita za mraba 250 bado linaweza kutosha kumudu nyumba ya vyumba vitatu.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *