NYUMBA NDOGO ZAIDI YA FAMILIA KUJENGWA.

Kuna watu wanahitaji kujenga nyumba za familia kwa sababu tayari wana familia kubwa lakini uwezo wa kujenga nyumba ni mdogo na hivyo wanahitaji nyumba ya ukubwa utakaogharimu kiasi kidogo zaidi cha gharama.

Kwa kawaida nyumba ya familia ya kiwango cha chini kabisa haipaswi kupungua chini ya angalau vyumba vitatu vya kulala, kimoja cha “master bedroom” chenye maliwato yake sambamba na sebule, jiko na stoo yake na “dining” ya kulia pamoja na maliwato ya umma.

NYUMBA YA VYUMBA VITATU

Nyumba yenye matumizi hayo ndani ndio nyumba ya kiwango cha kawaida kabisa kwa ajili ya familia lakini ili kuzidi kupunguza gharama basi vyumba hivyo vinapaswa kuwa vidogo vidogo zaidi ili nyumba yenyewe isigharimu eneo kubwa, malighafi nyingi wala kazi kubwa sana ya ufundi.

Nyumba ikiwa na matumizi machache zaidi ya hayo inakuwa sio nyumba ya kiwango cha familia tena kama familia za kawaida zinazohitaji kuwa na idadi sahihi ya vyumba vinavyotosheleza kwa matumizi sahihi ya familia.

NYUMBA YA VYUMBA VITATU

Kuzingatia hilo kutasaidia kuepuka kero nyingi za baadaye ikiwa ni pamoja na kutaka kuongeza ukubwa nyumba ambapo itapelekea gharama kubwa zaidi ya ile ya kujenga moja kwa moja idadi sahihi inayohitajika.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

6 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *