KWA MKOPO WA NYUMBA (MORTGAGE) WAPIGIE FIRST HOUSING FINANCE.

Wanaotoa mkopowa nyumba moja kwa moja kama mkopo wa nyumba ni taasisi ya kifedha ya First Housing Finance. Muhimu sana ni kufika katika ofisi zao kwa sababu sehemu kubwa ya kufanikisha kupata mkopo uko kwenye mazungumzo na makubaliano.

FIRST HOUSING FINANCE

First Housing Finance wanapatikana Posta Dar es Salaam katika barabara ya Barack Obama avenue ambayo zamani ilijulikana kama Ocean road karibu na inapokutana na barabara ya Ali Hassan Mwinyi maeneo ya Palm Beach.

First Housing Finance ni taasisi pekee inayoshughulika na mikopo ya nyumba peke yake ya aina ya “mortgage” ambapo kwa miradi mipya inaanza kwa kutoa asilimia 80% ya gharama zote.

FIRST HOUSING FINANCE

First Housing Finance ina riba ya mwaka ya asilimia 16% na marejesho yake yanaenda mpaka kipindi cha miaka 15 kuanzia wakati mkopo unapotolewa.

Unaweza kuwasiliana na First Housing Finance kwa namba +255 737 522 151

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *