HUDUMA BORA ZA USHAURI KITAALAMU KWENYE UJENZI ZINAHITAJI UWAJIBIKAJI WA KILA UPANDE.

Moja kati ya changamoto kubwa ambayo hasa wataalamu wa ushauri wa kitaalamu kwenye ujenzi hukutana nayo ambayo pia huchangia sana kupungua kwa ubora wa huduma hizi ni suala zima la malipo.

Kutokana na kwamba kuna kazi nyingi za kitaalamu ambazo wateja hukimbia bila kulipia huduma aliyopatiwa, hili limeondoa uaminifu kwa kiasi kikubwa kwa upande wa wataalmu kufanya kazi kabla ya malipo kwa sababu ya upande mmoja kushindwa kuwajibika.

UWAJIBIKAJI WA PANDE ZOTE MBILI NI MOJA YA MISINGI YA HUDUMA BORA

Kwa sababu hii, ili kazi ya kitaalamu iweze kufanyika kwa ubora na kwa muda uliopangwa inapaswa uwajibikaji kufanyika kwa pande zote mbili, kwamba mtoa huduma afanye ufafanuzi sahihi wa mchakato mzima kiasha alipwe na kazi ifanyike kwa viwango na ubora uliokusudiwa.

Ikiwa upande mmoja utashindwa kuwajibika kwa sehemu yake, hauna haki ya kulaumu upande mwingine kwamba umeshindwa kufanya kile kinachokusudiwa.

KILA UPANDE UNAPASWA KUWAJIBIKA KWA SEHEMU YAKE KUHAKIKISHA KILA KILIPANGWA KINAFANYIKA KWA USAHIHI

Kumekuwa na changamoto hii kubwa baina ya pande zote mbili ambayo imekuwa ikipelekea huduma kuwa katika viwango duni sana au kutofanyika kabisa lakini nguvu ya kukosekana kwa uwajibikaji imekuwa haionekani badala yake ni lawama kwa pande zote mbili.

Uwajibikaji unapokuwa kwa kila upande ambapo upande wa utaalamu unakuja na mapendekezo yake na baada ya majadiliano yanapitishwa kisha upande wa mteja unatekeleza kadiri ya makubaliano, basi ubora wa huduma unakuwa ni kitu cha uhakika zaidi na haki kwa kila upande.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *