UMUHIMU WA USIMAMIZI SAHIHI WA UJENZI HAUONEKANI, BALI MADHARA YA KUKOSEKANA KWAKE.

Changamoto kubwa iliyopo katika kuthamini ili kuweka kipaumbele kwenye huduma za usimamizi wa ujenzi ni umuhimu wake kutoonekana moja kwa moja na watu wachache sana kuweza kufikiria au kuona matokeo ya kuongezeka kwa thamani kwa sababu ya usimamizi sahihi.

MATOKEO YANAONEKANA LAKINI HUDUMA YA USIMAMIZI ILIYOLETA MATOKEO BORA HAIONEKANI

Kazi inapofanyika vizuri, kwa usahihi na kwa muda uliopangwa bila kuwepo changamoto yoyote kubwa ile nguvu ya usimamizi na umakini uliowekwa kufanikisha matokeo yaliyofikiwa huwa haionekani bali kinachoonekana ni matokeo ya mwisho peke yake na ndio maana huwa haipewi uzito unaostahili.

Hata hivyo pale usimamizi sahihi unapokosekana mambo huenda mrama sana na ubora wa kazi huwa ni kiwango cha chini sana, lakini licha ya hayo kutokea bado lawama huwa haziendi kwenye kukosekana kwa usimamizi sahihi bali kwenye ufundi au mafundi wazembe na wasio na viwango.

SIKU ZOTE KUNA NGUVU KUBWA YA UTEKELEZAJI ISIYOONEKANA ILIYOPO NYUMA YA KAZI YOYOTE YENYE UBORA.

Hivyo ni muhimu sana watu na hasa wateja kufahamu thamani inayoletwa na usimamizi sahihi ambayo huwa haionekani moja kwa moja na mara nyingi kupuuzwa licha ya kuongeza thamani kubwa sana na kuepusha hasara na usumbufu ukilinganisha na gharama zake.

Karibu kwa ushauri wa kitaalamu na usimamizi sahihi wa miradi ya ujenzi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *