KAZI YA UJENZI IPANGIWE MUDA WA KUFANYIKA KWA HARAKA KADIRI INAVYOWEZEKANA

Katika mchakato wa kupitia maombi ya zabuni za wakandarasi mbalimbali wa miradi ya ujenzi kuna vigezo kadhaa ambavyo hutumika katika kuchagua mkandarasi aliyeshinda zabuni na anayestahili kupewa kazi ya kujenga mradi husika.

Moja kati ya vigezo muhimu ambavyo huangaliwa ili kutoa zabuni husika ni pamoja na muda ambao mkandarasi huyo ameutaja kwamba atakuwa amemaliza kazi husika ya ujenzi.

Suala la muda limekuwa ni moja kati ya vigezo muhimu kwa sababu mradi kutumia muda mwingi sana katika kujengwa hupelekea hasara za namna nyingi sana. Kwanza kabisa na hasara ya muda ambayp moja kwa moja inaambatana na hasara ya fedha.

Kazi ya ujenzi inapomalizika kwa haraka maana yake jengo husika litaanza kutumika na ikiwa ni jengo la biashara maana yake litaanza kuingiza fedha kwa haraka n ahata ikiwa ni jengo la makazi maana yake litahamia haraka na hivyo gharama ya kutumia jengo lingine ambalo pengine linahusisha gharama ya kodi itakuwa imeokolewa.

Kazi ya ujenzi pia inapotumia muda mrefu sana kumalizika inapelekea matatizo mengine ikiwemo gharama zaidi kutumika kwenye ulinzi wa eneo la ujenzi, mkandarasi kutumia gharama zaidi kulipa watu kwa kukaa muda mrefu bila kazi kumalizika na hivyo kupungukiwa fedha na kulipua kazi, wataalamu wengine wa ushauri wa kitaalamu kuhitaji malipo zaidi kwa sababu ya mradi kuchukua muda mrefu.

Hizi ni baadhi ya sababu nyingi zinazotokana na kazi ya ujenzi kutumia muda mrefu kumalizika.

Karibu kwa huduma za ujenzi na utaalamu zinazofanyika kwa kasi kubwa na kwa ubora wa hali ya juu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *