CHANGAMOTO YA UMBALI KWENYE MIRADI YA UJENZI

Kwa miradi midogo ya ujenzi mara nyingi baadhi ya watu hoona kwamba pengine wanahitaji mtaalamu anayepatikana katika eneo au mji husika, ambapo mara nyingi ni kwa sababu ya kuhofia kwamba mtu anayetoka mbali atakuwa aidha na gharama kubwa au upatikanaji wake ni wa shida.

Ni kweli kwamba mtu anayepatikana karibu anaweza kupatikana kiurahisi kwa sababu ya ukaribu lakini kama ukizingatia ubora wa huduma umbali wa mtu anakotaka ni suala dogo sana na gharama ya ziada inayoambatana na mtu huyo kusafiri ni kidogo sana ukilinganisha na thamani ya huduma anayotoa.

Ikiwa mtu anapatikana nje ya mji au mji wa mbali tofauti na eneo la mradi ulipo lakini huduma zake ni za viwango vya juu zaidi basi ni chaguo sahihi zaidi kuliko kuangalia mtu wa mji husika asiye wa uhakika.

Miradi ya ujenzi kwa kawaida ni ya gharama kubwa hivyo umuhimu wa ubora wake haupaswi kuwekewa kikwazo kidogo kama cha umbali kwani ni kazi inayoweza kudumu hata kwa zaidi ya miaka 100.

Jambo la muhimu zaidi la kuzingatia ni ubora wa huduma kuliko kitu kingine chochote.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *