KUOKOA MUDA NA USUMBUFU SAJILI MRADI WA UJENZI KWA JINA LA KWENYE HATI.

Watu wengi hununua ardhi kwa ajili ya kuiendeleza kwa maana ya kujenga nyumba au jengo kwa matumizi fulani, ambapo mradi huu huhitajika kufanyika baada ya kukamilisha usajili wake kutoka kwenye mamlaka husika za ujenzi.

Lakini licha ya kuwepo kwa mkataba wa mauziano kati ya mmiliki wa sasa na mmiliki wa awali bado utakuta hati ya kiwanja ipo kwa jina la mmiliki wa awali, ambapo kubadilisha jina la umiliki ni jambo linalopitia mchakato na mlolongo kiasi.

Mradi wowote wa ujenzi unapaswa kusajiliwa kwa jina lililopo kwenye hati na hivyo ili mradi usajiliwe kwa jina la mmiliki wa sasa inatakiwa kwanza ufanyike mchakato wa kubadili jina la umiliki au kama sio hivyo mradi usajiliwe kwa jina la mmiliki wa awali lililopo kwenye hati.

Sasa mara nyingi, kwa sababu watu huwa hawalijui hili mapema huwa tunaokoa muda kwa kusajili mradi wa ujenzi kwa jina lililopo kwenye hati hata kama mmiliki wa sasa ana jina tofauti ili kwenda na kasi ya mradi kisha mchakato wa kubadili umiliki kwa jina la mmiliki wa sasa kuendelea.

Hata hivyo ikiwa mtu unahitaji mradi wa ujenzi usajili kwa jina lako au jina la kampuni yako, basi unahitajika kuhakikisha jina la umiliki kwenye hati ya kiwanja limefanyiwa mabadiliko kwa jina lako.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *