UJENZI WA NYUMBA NI SAFARI KWA VIJANA WALIO WENGI.

Kila kijana aliyefikisha umri wa kuanza kujitegemea hutamani kuwa na nyumba ya kuishi ambayo kwa watu wengi pia huwa ni ndoto yao ya miaka mingi tangu utotoni. Lakini tofauti na miaka ya zamani sana ambapo kujenga nyumba ilikuwa ni suala la kutumia teknolojia na malighafi zilizopo katika mazingira husika kwa usaidizi pia familia pamoja na majirani, ujenzi wa kisasa ni gharama kubwa na unahusika michakato mingi.

Hivyo tofauti na baadhi ya vijana ambao hawajafuatilia kuhusu masuala ya ujenzi, gharama ya kujenga nyumba ya kisasa ni kubwa sana ukilinganisha na kipato cha watu walio wengi na hasa vijana. Gharama ya kujenga nyumba moja ya kuishi ya vyumba vitatu kwa wastani inafika mara kumi ya gharama ya kununua aina ya magari ambayo vijana wengi wanamiliki.

Kutokana na ukubwa wa gharama hizo safari ya ujenzi kwa vijana wengi huja kuwa ni safari ndefu kwao tofauti na mawazo wanayokuwa nayo mwanzoni. Vijana wengi huwa hawaamini ukubwa wa gharama hizi za ujenzi mpaka wanapokuja kuanza kujenga lakini pia hujipa matumaini ya kukamilisha miradi yao ya ujenzi kwa muda mchache sana tofauti na inavyokuja kuwa katika uhalisia.

Ukweli ni kwamba kama nyumba unaijenga kwa fedha zako mwenyewe na sio kwa mkopo, na wewe ni kijana ambaye ndio unaanza maisha basi mara nyingi ujenzi huo utakuchukua muda mrefu ambao kwa wastani ni angalau kipindi cha miaka mitano.

Hili ni kutokana na ukweli kwamba gharama za ujenzi kwa wastani ni kubwa ukilinganisha na kipato cha vijana walio wengi hasa wenye wanaoanza maisha kutokea aidha shuleni au hata mtaani kwenyewe. Lakini jambo la muhimu ni mtu kuanza na kuweka bidii na fokasi kwenye kukamilisha taratibu mradi huo kwa sababu ukiamua kuendelea kuahirisha unaweza kujikuta umri unakwenda sana bila wewe kuanza ujenzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *