GHARAMA ZA UJENZI NI MACHAGUO YAKO MWENYEWE.

Gharama za ujenzi zimekuwa ni sehemu nyeti na muhimu sana kwa watu kufanya maamuzi juu ya miradi yao ya ujenzi kuanzia mwanzo kwenye kuandaa michoro mpaka kujenga kwa maana ya kuanzia kwenye huduma za ushauri wa kitaalamu, huduma za ujenzi mpaka vifaa vya ujenzi.

Watu wamekuwa wakiogopa sana gharama hizi na kuweka umakini mkubwa kwenye eneo lolote linalohusu gharama na kusikiliza kwa makini kiasi cha gharama ili kufanya maamuzi lakini bila kujua kwamba gharama zipo za viwango tofauti tofauti kulingana na machaguo yako.

Katika kila kifaa na kila hatua ya ujenzi kuna njia mbadala hata mara tano au zaidi wa huduma hiyo au kifaa hicho yenye utofauti wa gharama ambapo tofauti kati ya gharama ya chini kabisa na gharama ya juu kabisa inaweza kuwa hata mara tano au zaidi.

Hivyo kabla ya kuogopa gharama ni muhimu sana ukajua kwa undani kabisa utofauti unakuwa wapi, kipi ambacho utakipata au kukikosa kwa gharama hizo husika na kwa nini utofauti huu wa gharama unakuwepo kwa sababu licha ya gharama kusababishwa na machaguo pia husababishwa na ukubwa wa jengo ambao nao unahitaji kupimwa na kufahamu kwa nini umefikia hapo.

Hata hivyo watu wengi mara nyingi baada ya kuelewa kwa usahihi utofauti unaokuwepo wamekuwa wakibadili mawazo na kufanya maamuzi sahihi zaidi kwa kutumia akili badala ya kuongozwa na hisia na mara nyingi wamekuwa wakichagua kile ambacho wasingekichagua kama wasingefahamu utofauti uliopo na kuongozwa na hisia.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *