UKITAKA KAZI IFANYIKE KWA HARAKA NI MUHIMU PANDE ZOTE KUWAJIBIKA.

Kati ya vitu ambavyo huwaweka njia panda washauri wa kitaalamu pamoja na watu wengine ambao wanatoa huduma za ujenzi basi kinachoongoza huwa ni malipo. Ukiachana na uhalisia kwamba malipo huweza kulipwa kidogo lakini wakati mwingine malipo hucheleweshwa na wakati mwingine kutolipwa kabisa.

Suala hili limepelekea watu kupoteza imani katika kazi kwenye suala la malipo na hivyo kusababisha watu kukosa kabisa imani kwa kazi ambayo haijalipiwa na hivyo kupelekea kazi zisizolipiwa kutumia muda mrefu sana katika kufanyika kwa sababu ya wahusika kusubiri malipo.

Hivyo ikiwa mteja hajafanya malipo ya kazi husika anapoteza uhalali wa kulalamika kwamba kazi inachelewa kwa sababu suala la uwajibikaji linapaswa kuwa kwa pande zote mbili kutokana na kwamba wataalamu wengi ni wahanga wa kudhulumiwa na watu wasio waaminifu.

Lakini ikiwa mteja amewajibika kwa sehemu yake basi halafu upande wa mtaalamu ukawa ndio tatizo basi mteja anapaswa kulalamika na hata kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtaalamu ambaye ndio chanzo cha ucheleweshaji.

Kutokana na utamaduni wetu wa kuoneana aibu kwenye kuweka misimamo katika masuala ya fedha na kuwajibishana wengi tumekuwa wahanga wa eneo hili na kupelekea hata utendaji kazi wa viwango sahihi kushuka kwa kiasi kikubwa.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *