EPUKA KUFANYA MAKOSA HAYA KATIKA HATUA YA USANIFU YA KUANDAA MICHORO YA UJENZI.

Kwa kawaida binadamu tunatofautiana sana kwenye mambo mbalimbali hasa katika eneo la yale mambo tunayoyapenda na matamanio tuliyonayo. Kuna watu wengi shauku yao ya kuchukua hatua ni ndogo huku wengine wakiwa na shauku kubwa sana katika kuchukua hatua.

Ujenzi nao ni moja kati ya maeneo ambayo watu huvutiwa nalo na kila mtu huwa na matamanio yake pale linapokuja suala la aina ya nyumba au jengo analolitamani na hasa pale linapokuwa ndio jengo au nyumba ya ndoto zake.

Kutokana na watu kupenda sana kile anachokitamani hufikia hatua ya kutaka kushiriki katika kufanya vile anavyotaka yeye kifanyike na hapa ndipo changamoto kubwa hujitokeza. Pale mtu anapojaribu kushiriki katika kufanya kile anachotamani kifanyike na wakati mwingine kulazimisha kifanyike kwa kujumuisha kila anachotaka yeye mwisho wa siku kazi hiyo huharibika.

Mara nyingi kazi huishia kuharibika kwa sababu anayeifanya huwa ni yeye na sio tena mtaalamu na hivyo kama kuna mawazo au vitu vingine ambavyo mtaalamu wa kufanya anajua kanuni zake za ufanyaji ili kiweze kuleta mantiki utakuta hakifanyiki hivyo nah apo ndipo makosa makubwa hujitokeza na kuharibu kazi nzima. Hili sio rahisi sana kulielezea likaeleweka kwa usahihi sana lakini mara nyingi hutokea hivyo kwa sababu kuna kanuni huwa zinapuuzwa.

Kwa hivyo ni muhimu sana pale ambapo mtu unahitaji kufanya kazi yako hata kama unatamani sana ifanyike kwa namna fulani sio lazima kuwa na haraka sana bali ni muhimu kujieleza kwa usahihi sana na hata ikibidi kuleta picha au kuchora kwenye karatasi namna unavyotaka ifanyike kisha kuacha kazi hiyo ifanywe na mtaalamu husika. Atakapoleta kazi hiyo na ukaona kwamba haijafikia viwango unavyotaka au kuhusisha ubunifu uliokusudia ndipo unaeleza mabadiliko unayohitaji.

Kwa kufuata utaratibu huu mwisho utapata haswa ile unachotaka japo wakati mwingine kinaweza kupelekea kurudia mara mbili au tatu kadiri ya vile mlivyoweza kuelezana na kuelewana.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *