UJENZI UNA MAMBO MENGI SANA, UTAKUTANA NA MENGI USIYOYATARAJIA.

Changamoto kubwa iliyopo kwenye suala zima la ujenzi ni kwamba watu wanapofikiria kuhusu ujenzi huwa wanafikiria eneo moja tu ambalo ni kujenga. Yaani watu wengi wakifikiria kuhusu ujenzi huwa wanafikiria ile hatua ya mafundi kufanya kazi. Kosa hili la kimtazamo huwa linawagharimu sana watu kwa sababu baada ya kuingia kwenye mchakato mzima ndipo hukutana na mengi ya kushangaza na usumbufu mwingi tofauti na walivyotegemea mwanzoni.

Mchakato mzima wa kujenga unahusisha vitu vingi sana unavyovijua na usivyovijua na unavyovitarajia na usivyovitarajia hasa kwa mazingira ya nyakati za sasa. Kwa bahati mbaya zaidi ni kwamba vitu hivi sio rahisi kuvifahamu kama hutachukua hatua za makusudi za kujihangaisha kufahamu mpaka utakapokuwa unajenga wakati ambapo itakuwa imeanza kukugharimu.

Hivyo ni muhimu kuchukua juhudi za makusudi mapema kabla ya kuanza kufanya chochote kuhusu ujenzi kwa kuonana na watu wenye uzoefu watakaoweza kukujulisha kuhusu tahadhari zozote zinazoweza kutokea katika mchakato mzima wa ujenzi kuanzia tahadhari za kitaaluma, kifedha, kiufundi, kisheria, kijamii, kisiasa, kimamlaka, kimazingira na hata hali ya hewa.

Hili litakupa nafasi ya kujipanga kwa usahihi na kuanza kukabiliana na changamoto zote zinazoweza kujitokeza huku zile zisizotabirika ukiwa umejiandaa na uwezekano wake wa kutokea kitu ambacho kitasaidia kazi yake kufanyika vizuri bila kukutana na changamoto na hata baadhi ambazo zitajitokeza hazitakuwa za kushtukiza au kushangaza.

Sisi kama wajenzi ambao tumekusanya uzoefu mkubwa wa miaka mingi tuko kwenye nafasi nzuri pia ya kukupa ushauri ambao mwisho wa siku utakuja kushukuru na kujivunia kwamba ulifanya maamuzi sahihi yaliyokuepusha na changamoto na hasara zinazozuilika.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +2557171452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *