HIFADHI VIZURI MICHORO YA RAMANI ZAKO ZA UJENZI UTAKUJA KUIHITAJI BAADAYE.

Moja kati ya nyaraka muhimu ambazo unapaswa kuzihifadhi vizuri kwa sababu utakuja kuzihitaji baadaye ni pamoja na michoro ya ramani. Hii ni kwa sababu usipohifadhi vizuri michoro ya ramani ikapotea au kuharibika sana utakuja kuhitaji kutengeneza upya michoro ya ramani ya nyumba yako, kazi ambayo ni ngumu zaidi kuliko hata kutengeneza michoro mipya na ambayo inaweza kukugharimu sawa au zaidi ya gharama uliyotumia kuitengeneza mwanzoni.

Kazi ya kutengeneza michoro ya ramani ya nyumba ambayo ipo tayari inaanza kwanza na kazi ya kuchoro upya vipimo vyote vya nyumba hiyo katika kila kitu kwa usahihi kabisa, zoezi ambalo huitwa kwa lugha ya kitaalamu “documentation” kisha baada yah apo ndio kazi ya kuchora ianze, ambapo kazi ya “documentation” yenyewe tayari ni kazi kubwa na ngumu kabla ya kuanza kuchora upya.

Lakini uhitaji wa michoro ya ramani ya nyumba yako huwa ni mengi na katika nyakati tofauti tofauti za kipindi cha maisha ya nyumba hiyo. Kwanza mamlaka zinazohusika zinaweza kuja kuhitaji michoro ya ramani kwa sababu mbalimbali na itakulazimu uwapatie, lakini pia taasisi yoyote ambayo itahitaji kushughulika na nyumba yako kama vile kampuni za uthaminishaji wa thamani za majengo, mabenki, makampuni ya bima au hata watu wa mipango miji wanaweza kuhitaji michoro hiyo ikiwa wewe mwenye utahitaji huduma yao hiyo.

Muhimu zaidi pia ni pale utakapofika mahali na kuhitaji kufanya maboresho hususan ya kuongeza ukubwa wa nyumba yako ambapo ili kazi ifanyike kwa ubora na kuweza kukidhi mahitaji yanayotarajiwa itakulazima upate kwanza michoro ya maboresho ndio kazi iweze kufanyika nah apo ndipo utahitaji pia kuwa na michoro ya jengo hilo ili kumrahisishia kazi mtaalamu anayehitaji kufanya mabadiliko hayo, au hata wewe mwenyewe katika kufikiria kile ambacho ungeweza kufanya itakuwa rahisi zaidi kufanya maamuzi baada ya kuiangalia ramani yenyewe na kuona nini kinachowezekana kabla ya kumwita mtaalamu.

Hivyo ni muhimu sana kuhifadhi vizuri michoro yako ya ramani kwa matumizi ya baadaye kwa sababu kama hizo. Lakini kutokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika kuhifadhi nyaraka kwa dunia ya sasa ambapo teknolojia ni kubwa sana ni muhimu kuhifadhi nyaraka hizo katika mifumo yote yaani katika nakala ngumu(hardcopies) ambazo utahifadhi ndani ya nyumba, benki au kwenye taasisi nyingi unayoiamini pamoja na nakala tete(soft copies) ambazo utahifadhi kwenye barua pepe au kwenye eneo lingine lolote la uhakika mitandaoni.

Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kwamba unapofanya kazi ya michoro ya ramani uhakikisha mtaalamu aliyekupatia anakukabidhi nakala ngumu pamoja nan akala tete katika mfumo wa pdf, na ikiwa kwa sababu yoyote ile imeshindikana kupatikana nakala tete basi ni muhimu ukafanya (scanning) ya nyaraka hizo kupata nakala tete katika picha na kuzihifadhi.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *