KURAHISISHA ZOEZI LA UJENZI WA NYUMBA YAKO WEKA MUDA MWINGI WA KUSHUGHULIKA NAO.

Kati ya vitu ambavyo vitakugharimu, kukupotezea muda sana na kuwa kero sana kwenye mradi wako wa ujenzi ni vikwazo utakavyokutana navyo kwa ghafla utakapokuwa unafuatilia mambo mbalimbali ambavyo hukuvitegemea na vitakavyokuwa vinahusisha usumbufu mkubwa sana ambao hukuutegemea pia na kuchelewesha sana mradi wako tofauti na ulivyokuwa unapanga na pengine hata kukuingiza hasara ya fedha na muda.

Hii ni kutokana na kwamba mradi wowote wa ujenzi ambao unalazimika kuidhinishwa na mamlaka za ujenzi pamoja na taasisi na idara nyingine za serikali kama vile halmashauri za miji, manispaa na majiji na idara zake, ni lazima utakutana na usumbufu mwingi sana na ambapo ni ngumu sana kutokutana na usumbufu wowote iwe ulikuwa na mpango wa kupata vibali vya mamlaka hizo au umelazimishwa na watu wa mamlaka husika baada ya kukuona ukijenga.

Hivyo jambo la muhimu na kipaumbele cha kwanza kabisa ni kuanza ufuatiliaji wa vitu hivyo mapema sana kabla hata ya kuwa “serious”na mradi wenyewe ili unapofuatilia usijikute unalazimika kufanya vitu vingine kwa sababu ya kuwa na haraka, lakini pia ni muhimu ili kufahamu gharama mbalimbali za ziada ambazo utapaswa kuzilipa mapema na muda ambao utachukua.

Kwa mfano kufanya mabadiliko ya matumizi ya kiwanja ni zoezi linahusisha mchakato mrefu ikiwemo kuweka tangazo katika eneo la kiwanja chako litakalokuwepo hapo kwa angalau mwezi mmoja ili kama kuna mtu anayepingana na maamuzi hayo afikishe malalamiko yake kwenye mamlaka husika, ikiwa ni sehemu tu ya hatua za kuelekea kuruhusiwa kufanya mabadiliko hayo lakini pia utakutana na urasimu mwingine mbalimbali wakati unaendelea na mchakato huo.

Sasa kama hata sasa uko kwenye mipango ya kuanza ujenzi wa mradi wowote lakini bado nasubiria ni muhimu sasa hivi ukaanza kufuatilia hata kama utakuja kuanza ujenzi huo baada ya mwaka mmoja au zaidi kutoka sasa, kwani utaweza kujifunza mambo mengi mapema na kuna hatua nyingine unaweza kuzichukua sasa hivi ili kuokoa muda utakaopoteza wakati unataka kuanza ujenzi huo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *