UKUBWA WA VYUMBA UNAVYOHITAJI.

Mara nyingi sana wateja wengi tunaokutana nao huwa hawana mawazo ya ni ukubwa gani wa vyumba na maeneo mengine ndani ya nyumba zao wanaouhitaji. Hii huwa inakuwa changamoto kidogo kwa mtaalamu kwa sababu ni vigumu kubashiri ukubwa ambao mteja anauhitaji kwa sababu inakuwa vigumu kujua uzoefu wake wa eneo analoishi na namna anachukulia ukubwa aliouzoea.

Changamoto huwa inakuja pale ambapo ujenzi unakuwa umekamilika halafu mteja ameanza kutumia nyumba yake ndipo anapogundua aidha vyumba vya nyumba yake ni vidogo kupita kiasi au ni vikubwa kupita kiasi na ndipo anaona kwamba kazi yake haikufanyika vile alivyopenda ifanyike. Hapa lawama huwa zinaenda kwa mtaalamu aliyefanya ramani hiyo kwa sababu aliamua kufanya vile alivyoona yeye inafaa badala ya mteja mwenyewe kushirikisha uzoefu wake.

Kutokana na kwamba kila mtu anayetaka kujenga huwa kuna nyumba ambayo anaishi kwa wakati huo, basi hiyo ndio inayopaswa kumsaidia mteja kujua anataka nini. Nyumba ambayo mtu anaishi kwa wakati husika na uzoefu wake juu ya ukubwa wa nyumba ndio kipimo sahihi cha ni ukubwa kiasi gani anaouhitaji kwenye nyumba anayotaka kujenga kwa wakati huo.

Hivyo ni muhimu kwamba mteja anapohitaji kufanyiwa kazi ya kitaalamu ya michoro ya ramani ni aidha anapaswa kuangalia ukubwa wa vyumba vya nyumba anayoishi na kuamua kama anahitaji vyumba vikubwa zaidi ya hivyo anavyoishi kwa sasa au anahitaji vyumba vidogo zaidi. Kisha ikibidi mtaalamu anayeifanya michoro ya ramani ya nyumba hiyo kuitembelea na kuhakiki vipimo kisha kuamua kama itabidi aongeze zaidi ya hivyo au apunguze zaidi kadiri ya mahitaji ya mteja.

Kwa utaratibu huu ni vigumu sana baadaye baada ya nyumba kuwa imekamilika mteja kuja kulalamika kwamba vyumba ni vidogo au vikubwa kwa sababu vimefanyika kadiri ya uhitaji wake kutoka kwenye uzoefu wa nyumba na vyumba vya nyumba aliokuwa anaishi hapo kabla. Hii ni kwa sababu ni vigumu kubashiri ukubwa ambao mtu anauhitaji pasipo kuwa na vipimo vinavyotokana na uzoefu wa matumizi ya vyumba kwa mteja husika.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *