KUPATA KIBALI CHA UJENZI JINA LA KWENYE HATI LINAPASWA KUWA JINA LA MRADI.

Hili ni suala ambalo limekuwa halifahamiki vizuri kwa wengi lakini ni suala muhimu sana kwa watu kujua kwa sababu watu wengi wanamiliki viwanja ambavyo haviko kwa majina yao kwa sababu bado hawajafanya mabadiliko ya jina kutoka kwa jina la aliyemuuzia kiwanja kwenda kwa jina lake. Hivyo mtu anapofikia kujenga na kutaka jina la mradi lisomeke kwa jina lako ndipo anapokutana na uhalisia kwamba hilo halitawezekana katika kupewa kibali cha ujenzi.

Ili kupata kubali cha ujenzi jina lililopo kwenye hati ndilo jina ambalo hutambulika na mamlaka husika na hivyo mradi hupaswa kusajiliwa kwa jina lililopo kwenye hati ya kiwanja bila kujalisha kama ndio jina la mmiliki au la. Hii ni kwa sababu usajili wa mradi wa ujenzi huambatana na nyaraka za hati ya kiwanja ambazo ndio huwa zinatumika katika kuhakiki eneo pamoja na taarifa za umiliki na hivyo taarifa zikiwa zinakinzana hapo huonekana kama kuna udanganyifu na hivyo mradi kuzuiwa usajili.

Hivyo unapofikia hatua ya kuamua kujenga na ikiwa unataka jina la mradi liwe ni jina lako basi inabidi jina lililoko kwenye hati yako liwe ni la kwako. Kama sio hivyo basi inakubidi aidha ubadilishe kwanza jina la umiliki kutoka kwenye jina la mtu aliyekuuzia kwenda kwenye jina lako au kama una haraka basi ukubali kusajili mradi kwa jina la yule aliyekuuzia lililopo kwenye hati ya kiwanja kisha ndio uendelee taratibu na mchakato wa kubadilisha jina la umiliki.

Hata hivyo kama hutajali jina lililopo kwenye hati linaweza kutumika kama jina la kusajilia mradi husika wa ujenzi na mambo mengine yakafanyika bila usumbufu wowote kisha wewe baadaye ukaja kubadilisha jina hilo bila tatizo lolote, au hata ukaendelea na mchakato wa kubadilisha jina la umiliki wa kiwanja mara baada ya kupata kibali cha ujenzi na kuanza ujenzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *