FAIDA NA HASARA ZA KUJENGA KIENYEJI.

Kama ilivyo kwa taaluma nyingine yoyote kuna kanuni za kufuata ambazo hutoa mwongozo sahihi wa kufanikisha jambo fulani kwa usahihi na kwa viwango bora vinavyokubalika. Na ikiwa kanuni hizo hazikufuatwa basi kazi husika au mradi husika hupata madhara fulani ya kuwa na walakini au hitilafu fulani ambayo husababisha usumbufu fulani kwenye kazi husika au mradi husika.

Mara nyingi ujenzi wa kienyeji katika utekelezaji wake hupuuza mambo mengi ya msingi na muhimu katika kazi husika kwa sababu mbalimbali lakini kubwa na muhimu ni kukosekana kwa wataalamu wenye uelewa wa madhara husika na watakaoweka umakini mkubwa ili kuhakikisha uzembe huo haufanyiki kwa sababu ya madhara hayo.

Kwa mfano jengo la ghorofa lililoanguka huko Goba na kuua watu wanne na kusababisha majeruhi wengine wengi ni matokeo ya ujenzi wa kienyeji ambao umepuuza baadhi ya mambo muhimu kutokana na wahusika waliokuwa wanatekeleza ujenzi huo kukosa uelewa sahihi wa madhara ya mambo waliyopuuza na hivyo kuwa na ujasiri wa kupuuza kwa kutokujua madhara makubwa yanayokuja mbele yake.

Lakini hata hivyo madhara hayapo kwenye jengo kuanguka peke yake bali yapo pia kwenye mpangilio mbovu wa ndani wa jengo unaopelekea matumizi ya jengo kuwa na changamoto sana au yasiyofurahisha watumiaji. Madhara yapo pia kwenye muonekano wa nje wa jengo ambayo yanasababisha jengo kuwa na taswira mbaya na kushindwa kuwavutia watumiaji.

Hata hivyo kabla hatujalaumu moja kwa moja tuangalie ni kwa nini sasa watu waamue kujenga kienyeji wakati wataalamu wabobezi wanapatikana. Na hapa sasa ndipo unakutana na ile faida wanayoitafuta. Faida za ya kujenga kienyeji ni urahisi wa gharama ambao kila mtu ndio huwa anaukimbilia na ndio huwa ni kipaumbele chake cha kwanza kabla ya kufikiria mambo mengine muhimu.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *