USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 20 SAFARI YA MAFANIKIO KUMILIKI MAJENGO MAKUBWA

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Gail Wynand alizaliwa kwenye familia maskini sana na kukulia kwenye mitaa ya watu maskini. Mama yake alifariki akiwa na umri wa miaka 2 na baba yake alifariki akiwa na umri wa miaka 16. Alikuwa ndiye mtoto pekee wa kiume katika familia.

2. Gail Wynand alijiingiza kwenye genge la wahalifu tangu akiwa na umri mdogo sana wa miaka 12. Na haikuchukua muda mrefu alikuwa kiongozi wa genge la wahalifu. Hii ilitokana na kwamba alikuwa na uwezo mkubwa kiakili na ubunifu hivyo alijenga ushawishi kwa haraka.

3. Gail Wynand hakuwahi kwenda shule kabisa bali alijifundisha mwenyewe kusoma na kuandika. Wazazi wake pia hawakuwahi kwenda shule na wala hawakuwa wanahudhuria kanisani.

4. Gail Wynand alipenda sana kusoma na kufahamu vitu mbalimbali. Alijifunza kila kitu kutoka kwa wataalamu husika na kuongeza sana maarifa kupitia kusoma vitabu. Alijaribu kufahamu kila kitu.

5. Gail Wynand alikuwa ndiye kiongozi pekee wa genge la wahalifu aliyeagiza kuvamiwa kwa duka la vitabu na kuporwa vitabu, kitu ambacho hakuna kiongozi wa genge la wahalifu anaweza kufanya.

6. Baada ya baba yake kufariki Gail Wynand alifikiria sasa ni wakati muafaka wa yeye kufikiria jambo sahihi la kufanya katika maisha yake.

7. Gail Wynand alianza kazi ya kuuza magazeti mitaani. Baadaye aliomba kazi ya kujitolea kwenye ofisi za habari akawa anafanya kazi ya kujitolea bila kulipwa chochote.

8. Gail Wynand alikuwa analala mitaani lakini haikuchukua muda mrefu alifanikiwa kupewa mkataba wa kazi.

9. Aliendelea kufanya kazi kwa bidii na kupanda ngazi akizidi kufanikiwa mpaka akafikia kuinunua kampuni yenyewe na kuimiliki.

10. Baadaye alibadilisha jina la gazeti hilo maarufu na kuliita “The New York Banner” au “The Banner”.

11. Gail Wynand aliendelea kuwa mwekezaji katika maeneo mengine kama vile majengo n.k.

12. Ellsworth Toohey anafika nyumbani kwa Gail Wynand ambaye ni boss wake kupitia jarida la “The Banner”, kujaribu kuzungumza naye. Ellsworth Toohey anajaribu kumshawishi Gail Wynand kuwakutanisha na Dominique ambaye yeye Ellsworth Toohey anamwita Mrs. Peter Keating.

13. Gail Wynand anakataa pendekezo la Ellsworth Toohey la kukutana na Dominique lakini Ellsworth Toohey anajaribu kumshawishi zaidi kufanya hivyo. Hata hivyo kupitia ile sanamu ya Dominique iliyochongwa na Steven Mallory Gail Wynand anajaribu kufikiria mara mbili.

14. Gail Wynand anamwambia Ellsworth Toohey yeye anahitaji kukutana na mtu aliyechonga sanamu hiyo na sio huyo mwanamke. Ellsworth Toohey anajifanya amemsahau, Gail Wynand anamwambia sio kweli, Ellsworth Toohey anajifanya kama anajaribu kukumbuka lakini anasema hamkumbuki. Anamshawishi akutane na Dominique lazima atakuwa anamfahamu mchonga sanamu yake.

15. Gail Wynand anaonekana kukubali kwamba atakutana na Dominique.

16. Peter Keating na Dominique wanatumia muda mwingi pamoja wanahudhuria sherehe mbalimbali pamoja. Dominique anaonekana kuwa mtiifu kwa Peter Keating na anamwambia kabisa yeye atamsikiliza na kufuata maagizo yake, na kumuunga mkono kwa kile atakachotaka kufanya.

17. Peter Keating anajivunia sana kuwa na Dominique kama mke wake na anajivunia kumwambia kila mtu na kufurahia vile watu wanamwonea wivu.

18. Peter Keating anamwambia Dominique kwamba anahitaji kujenga nyumba kubwa ya kisasa nje ya mji kwa sababu uwezo anao, Dominique anamwambia kama ndivyo anavyohitaji ni sawa.

19. Lakini hata hivyo Peter Keating bado hajawa na ujasiri wa kutosha kuthubutu kufanya mapenzi na Dominique licha ya kulala naye pamoja.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *