MSIMAMIZI WA UJENZI AONYESHE MAJUKUMU YAKE NA KUTOA RIPOTI YA KAZI YAKE.

Katika miradi ya ujenzi iwe mteja ameweka mkandarasi kamili au msimamizi peke yake, yule msimamizi aliyewekwa anapaswa kufanya kazi inayoeleweka na kupimika. Yaani msimamizi au mkandarasi anapaswa kupeleka mpango wake mzima wa kazi ambayo anaenda kuifanya tangia mwanzo mpaka mwisho. Mpango kazi huo utaonyesha majukumu yake anayokwenda kufanya na matokeo yanayotegemewa sambamba na muda anaokwenda kuutumia pamoja na wakati atakaokuwa anafanya jukumu husika. Utaratibu huu ni utaratibu ambao utarahisha sana kazi kwa pande zote mbili na kuondoa sintofahamu nyingi ambazo zinaweza kujitokeza.

Lakini kwa bahati mbaya hilo silo linalofanyika, katika miradi mingi wasimamizi wa ujenzi hufanya kazi kwa mtindo huru, “freestyle” bila ya kuwa na kinachomwongoza wala kueleza ni matokeo gani yanatarajiwa kwenye kazi yake. Imekuwa kwamba msimamizi anafika katika eneo la ujenzi kusimamia mafundi wake au kuangalia kilichofanyika na kutoa maelekezo, marekebisho na maboresho kisha kutoa taarifa ya kufika kwenye ujenzi kisha kuondoka. Mtindo huu wa aina ya mtindo huru umekuwa ukipelekea makosa mengi kufanyika kwa sababu ya kutopewa umakini kwani sio kila kitu kitakumbukwa kwenye kichwa cha mtu mmoja. Mambo mengi muhimu yamekuwa yakisahaulika au wakati mwingine kupuuzwa kwa sababu hayawekwa rasmi kwenye mpango kimaandishi kwamba yatafanyiwa kazi na kufika wapi.

Sasa kinachopaswa kufanyika ni msimamizi wa ujenzi mzima bila kujalisha kama amekabidhiwa mradi wote na majukumu yote au kama amepewa kazi ya kutoa huduma ya kiufundi peke yake kutengeneza mpango kazi wa kazi yote kipengele kwa kipengele juu ya yale yanayokwenda kufanyika na ni matokeo gani watu wayategemee. Akishamaliza kuandika atatoa nakala na kuipeleka kwa mteja mwenye jengo kumwonyesha maeneo anayokwenda kusimamia na matokeo yanayotarajiwa. Yeye msimamizi atabaki nakala moja ambayo ndio anayokwenda kuifanyia, kuandika ripoti nzima ya kazi kadiri kazi inavyoendelea na kuiwasilisha kwa mteja ambaye atapaswa kuona thamani rasmi ya huduma yake ya usimamizi anayotoa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *