UKIFANYA MAAMUZI KWENYE UJENZI KIENYEJI UTAICHUKIA NYUMBA YAKO.

Baada ya hatua ya michoro ya ramani kukamilika kisha mradi wote unaoenda kufanyika kuwa wazi, watu wote wanategemea kuona utekelezaji wa mradi huo ambao unaunda kufanyika kama jinsi michoro ya ramani inavyoonyesha. Mteja na wadau wengine wanakuwa wameliona jengo na uzuri wake na hivyo wanatarajiwa mwishoni kuona kile kilichofanyika kwenye michoro. Na kweli kazi ikifanyika kimalimifu kwa usahihi mwisho wa siku kweli jengo litakalojengwa ni kama michoro inavyoonyesha kwa muonekano, ukubwa na mpangilio.

Hata hivyo kwa bahati mbaya kwa kuwa binadamu ni viumbe wa kubadilisha mawazo kila mara bila hata wao wenyewe kutegemea, hili sio suala linalotokea hivyo mara zote. Mara nyingi unakuta vitu vingi vinabadilishwa wakati ujenzi unaendelea bila kushirikisha utaalamu wala kujali madhara ya maamuzi yanayoenda kufanyika na mwisho kujikuta kile kilichodhamiriwa kufanyika kimekuwa tofauti kabisa na mwanzoni. Na hili hutokea kwa sababu wanaofanya maamuzi hawafanyi kwa kuzingatia ushauri na kanuni za kitaalam bali kutumia utashi wao wenyewe wakati hawana uzoefu wala uelewa wa yale mambo ya msingi katika taaluma za ujenzi.

Matokeo yake ni kwamba unaweza kukuta kwamba jengo mwanzoni lilikuwa na mwonekano mzuri na unaovutia sana kwa namna lilivyokuwa limepangiliwa, lakini kwa sababu ya kufanya maamuzi ambayo mtu anatamani kuona ikiwa au kuvutiwa nayo kwa namna nyingine yoyote basi kila kitu kinabadilika. Baada ya ujenzi kukamilika ndio wanaanza kushangaa mbona lile jengo zuri tuliloliona mwanzo na kulitarajia halipo tena bali tuko na jengo lisilo na mvuto wala umaridadi ule wa mwanzo tuliouona kwenye puicha, Hapo mteja anaanza kuona kama ametapeliwa au kuhujumiwa na kuichukua nyumba yake ambayo ameigharamia fedha nyingi sana kuikamilisha.

Kumbe wakati mwingine makosa aidha alifanya yeye au mtu mwingine wa karibu ambaye alimruhusu aamua vile itakavyokuwa wakati hana uzoefu na haoni haja ya kumshirikisha mtaalamu kwa sababu hawazi kwamba maamuzi yasiyo sahihi yataharibu jengo hilo. Jambo hili limetokea mara kwa mara sana kwani wakati mtaalamu anajipanga ili jengo liwe zuri zaidi lakini anakuta tayari maamuzi yameamuliwa kienyeji bado yanabaki kuwa maamuzi licha ya kwamba yanapelekea kupungu za thamani ya jengo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *