UJENZI WA NYUMBA KIJIJINI.

Watu wengi hasa katika nchi zinazoendelea ni aidha wa wametokea vijiji au wazazi wao walitokea vijijini hivyo wana makazi ya kurithi katika maeneo ya vijijini. Sasa kutokana na uhalisia huo watu wengi wamekuwa wakisukumwa kujenga nyumba za kuishi katika maeneo waliyotokea hata kama hawaishi maeneo haya kwa muda wote wakiwa na sababu mbalimbali. Kuna wengine wanafanya hivyo kwa kufuata utamaduni walioukuta ukiendelea kutoka kwa watangulizi wao, wengine wanafanya ili kuweka mazingira ya nyumbani kwao kwa asili salama ili yanapotokea matukio muhimu ya kijamii kuwa na makazi bora watakayotumia wakati wakihudhuria matukio hayo. Lakini wengine pia hufanya hivyo ili kuwa na makazi mazuri na kuonyesha ufahari kwa ndugu zao na watu wa jamii yao kuwa wao ni watu wenye maendeleo makubwa na waliopiga hatua sana.

Hizo ni sababu mbalimbali za watu kujenga vijijini kwao, hivyo leo ningependa kuzungumiza mambo ya kuzingatia unapokwenda kujenga kijijini kwetu. Kwanza kabisa usifanye mradi wa kijijini ilimradi kwa sababu unahisi sio wa muhimu sana kupewa kipaumbele kwa sababu mbalimbali. Sababu mbili kubwa ni kwa nini uzingatie ubora na utaalamu katika kujenga vijijini ni moja unapaswa kujua wakati wewe unajenga kiholela kwa sababu ni kijijini kuna wenzako wengi wanajenga nyumba bora sana na makini kijijini kwa kuzingatia ubora na utaalamu kitu ambacho kitafanya nyumba yako ionekane ni kitu mbele za nyumba za watu wengine wengi makini na wanaoongezeka kila wakati. Sababu ya pili ni kwamba vijiji vingi leo hii vinakuwa kwa kasi sana kuelekea kuwa miji na baada ya miaka kadhaa au miongo michache kuna vijiji vingi vitakuwa miji kamili hivyo kama hukujenga nyumba yenye ubora nyumba yako itapitwa na wakati haraka na kuleta aibu hivyo kuhitajika kulazimika kuibomoa na kujenga nyumba yenye hadhi.

Jambo jingine la kuzingatia unapokwenda kujenga vijijini ni usichukue mtu yeyote akujengee nyumba yako kwa sababu tu anaishi maeneo ya karibu na nyumbani kwa sababu ni mtu wa nyumbani na pengine atakuwa ni wa gharama ndogo. Badala yake tafuta mtaalamu sahihi wa kujenga nyumba yako hiyo ambaye atakufanyia kazi bora itakayokubalika na kuwa gumzo kabisa hapo kijijini kwani hiyo yenye itakuongezea heshima na thamani yako kubwa maeneo ya kijijini kwenu. Lakini pia kwa kuwa siku hizi kuna taasisi na mamlaka nyingi za maendeleo ya vijijini kuna urasimishaji mkubwa wa maeneo ya vijijini katika ili kuzingatia viwango mbalimbali kimiundombinu na kimakazi hivyo ikiwa ujenzi wako haujafanyika katika viwango sahihi huwezi kujua ni wakati gani mamlaka zitafika kuhoja na kujikuta umeingia kwenye matatizo makubwa au kwenye hasara kubwa.

Tutaendelea kujadili mada ya ujenzi vijijini katika makala zinazofuata.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *