SAIKOLOJIA YA KUMWAMINI MTU INAYOGHARIMU SANA WATU KWENYE UJENZI.

Binadamu tumeumbwa na hali fulani ya kuamini watu wetu wa karibu pale wanatuambia au kutuhakikishia jambo. Suala hili lilikuwa ni jambo la muhimu sana kwetu wakati tukiwa tunaishi ndani ya jamii kwani lilisaidia kuepuka hatari nyingi wakati huo ambapo tabia hiyo imejengeka kabisa ndani yetu kiasi kwamba ina nguvu ile ile iliyokuwa nayo zama za kale kabisa. Hata hivyo kwa sasa ambapo dunia ina mchanganyiko wa watu na watu wenye nia na malengo mbalimbali tofauti tofauti baadhi ya watu wanaitumia vibaya na kusababisha maumivu makubwa kwa wengine.

Tabia hii ni mtu kuaminiwa kwa neno la mdomo na kupewa imani ambayo pengine haimstahili kisha kufanya mambo ambayo hayakuwa sehemu ya makubaliano na kupelekea matatizo na usumbufu kwa wengine. Kwenye ujenzi na hasa kwenye kazi za kiufundi ambazo mara nyingi watu hupewa imani kwa neno la mdomo kumekuwa na changamoto ya watu kutumia nafasi hiyo kukosa uaminifu na kuharibu kazi za wengine au kufanya wizi na ubadhirifu.

Hata hivyo changamoto zaidi ni kwamba mtu anaweza kuwa na uwezo mzuri lakini akapewa kazi na kuharibu kwa sababu ya tamaa au ushawishi mbaya. Ikiwa mtu hajazoea kufanya kazi kwa kujisimamia halafu kwa mara ya kwanza akapewa kazi kubwa na yenye maslahi, anaweza kubadilika na kukosa uaminifu kwa sababu au ya tamaa au ushawishi mbaya na akaishia kufanya mambo ya hivyo yasiyofaa na kuumiza sana watu.

Hivyo kitu muhimu na kizuri cha kufanya kwanza ni kuwa makini na mtu unayeunganishwa naye hata kama umepewa na mtu wako wa karibu bado unapaswa kuongeza umakini sana kwenye kudili naye, pili ni kama una nafasi ya kujihakikisha ubora na uaminifu wake ujaribu kufuataili pia. Mwisho na muhimu sana ni kuipangilia kazi kwa namna ambayo haitakuwa na hasara kubwa mpaka inapofika pale unapokuwa umejiridhisha kwamba mtu huyo ni mwaminifu na mwenye uwezo.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *