USIMAMIZI WA KAZI YA UJENZI SITE UNAHUSISHA UKAGUZI WA KINA KWA KILA HATUA.

Miradi ya ujenzi bila kujalisha ni midogo au mikubwa ni kati ya miradi ambayo huwa na makosa mengi sana katika utekelezaji wake. Miradi hii huambatana na makosa mengi sana ya kiutendaji kwa sababu inahusisha taarifa nyingi sana za kwenye michoro ya ramani kwenye kuitekeleza ambayo kutokana na kukosa umakini katika au ugumu kwenye ufanyaji. Hivyo wakati mshauri wa kitaalamu anapotembelea eneo la ujenzi anapaswa kutumia muda mwingi kukagua kila kitu na wakati mwingine hata kupima usahihi wake kwa vipimo kwani bila kuweka umakini atajikuta anaacha makosa mengi nyuma yake.

Kwa maana hiyo sasa ili kuhakikisha hakuna makosa mengi yanayoachwa nyuma mshauri wa kitaalamu katika kutembelea site hiyo atatakiwa kutumia muda mwingi sana katika eneo la ujenzi ili kuhakikisha amekagua kila kitu kwa usahihi na kwa kina. Kazi ambayo inafanya na mshauri wa kitaalamu katika ukaguzi wa hatua mbalimbali na kutoa mapendekezo ni kazi ya thamani na inayokwenda kuokoa gharama kubwa na kuongeza sana thamani ya mradi na jengo husika hivyo sio kazi ya kupuuza au kutochukulia umuhimu. Na hili linajionyesha wazi kupitia makosa mengi ambayo hupatikana katika eneo la ujenzi kwa njia hii.

Jambo la muhimu kuzingatia ni kwamba katika ukaguzi kila utaalamu unapaswa kufanya ukaguzi wa eneo lake la kitaalamu ili kuhakikisha ubora na uhakika wa eneo husika unazingatiwa na kutoa mapendekezo. Ukaguzi wa kina utahakikisha kwamba kilichofanyika na kinachoendelea kufanyika kinakuwa katika viwango bora sana na sahihi na hakuna hasara kubwa ya kubomoa na kurudia kazi inayokwenda kujitokeza. Ikifanyika kwa namna hiyo basi kazi itakuwa nzuri na mwishoni makosa na hasara vitakuwa ni kidogo sana.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *